Microsoft wamekuja na apps kadhaa kwa ajili ya android na sasa wamekuja na app ya kengere (alarm), Mimicker Alarm, isiyonyamaza hadi ufanye mambo kadhaa.
Kuna apps nyingi sana za alarm kwa ajili ya watu wenye usingizi mzito, yaani wagumu kuamka. Unaweza kusoma makala yetu ya muda kidogo kuhusu apps za alarm bora zaidi lakini kwa sasa tunaamini ata app hii inastahili kuwa kwenye orodha hiyo.
Kupitia programu yao ifahamikayo kwa jina la Garage ndio wazo na utengenezaji wa app hiyo ulikuja.
Garage ni programu inayowapa wafanyakazi wa kampuni hiyo nafasi ya kukutana pamoja na kufanikisha mawazo mbalimbali kuwa mradi kamili na kufanyiwa kazi.
App hii itahakikisha unaaamka kupitia wewe kushiriki katika uchezaji wa gemu. Unaweza kuchagua aina ya mchezo unaotaka kucheza wakati wa kuamka wakati unapoweka alarm.
Michezo hiyo ni pamoja na;
- Kuonesha kitu na wewe kutakiwa kupiga picha kitu chochote karibu yako chenye rangi kama hiyo. App hiyo kupitia teknolojia ya utambuaji itatambua kama rangi hiyo ni sahihi, na kama si sahihi basi alarm hiyo itaendelea kuita.
- Piga picha ya selfie. Chaguo lingine litakuwa ni kukuitaji wewe kupiga picha ya selfie katika ‘pozi’ flani, mfano tabasamu n.k
- ‘Tongue twister’ – utapewa sentensi ngumu kidogo kutamka na utatakiwa kuzitamka kwa usahihi.
Mpangilio (setting) wa nyongeza ni pamoja na kuchagua ata baada ya kupitia zoezi (mchezo) lolote hapo juu lazima utume matokeo yake kwa marafiki kupitia mitandao ya kijamii na kama utafanya hivyo alarm itaita tena kama kawaida.
Kwa sasa app hiyo inapatikana kwa watumiaji wa Android, app nzima inachukua takribani MB 21 na inaweza kupakuliwa kwa simu zenye Android 4.1 KitKat na kuendelea. Toleo la iOS lipo njiani.
No Comment! Be the first one.