Kwa kifupi tunaweza kusema kampuni ya Microsoft inakuja kwa nguvu zake zote kuweza kudumu na kufanya vizuri katika soko la simu janja.
Microsoft wameonesha ubavu huo kupitia simu yao mpya ya Lumia 950 waliyoitambulisha masaa machache yaliyopita.
“inasifa nyingi za ubora wa hali ya juu ata pale ikilinganishwa na matoleo ya simu Za Samsung Galaxy S6 na iPhone 6S.”
Kwa nini Lumia 950 ni ya kipekee?
Kwa ufupi inasifa nyingi za ubora wa hali ya juu ata pale ikilinganishwa na matoleo ya simu Za Samsung Galaxy S6 na iPhone 6S.
Kioo (Display)
Simu hiyo inakuja na kioo cha inchi 5.2 kilichojaa pixels za kutosha (2,560 x 1440). Teknolojia nyingine spesheli inayokuja katika suala la kioo na teknolojia ya kusaidia kupooza simu hiyo kuzuia upataji wa joto kali.
Kamera
Simu ya Microsoft Lumia 950 inakuja na kamera ya Megapixel 20 ikiwa na sifa ya PureView. Lensi za kamera hiyo pia zinakuja na teknolojia ya kisasa zaidi katika kuhakikisha video na picha unazochukua ata pale unapokuwa unatetemeka au kupiga kitu kilichokwenye mwendo mkali kutokea katika kiwango kizuri bila tatizo lolote. Kamera hiyo inakiwango kikubwa kabisa cha kiwango cha ubora wa video wa 4K.
Diski Ujazo
Simu hiyo ina diski ujazo wa GB 32, pia inakuja na eneo la kuweza kutumia memori kadi, na utaweza kutumia hadi memori kadi (SD Card) ya ukubwa wa TB 2 bila tatizo lolote – memori kadi za ukubwa huu inasemakana zitaanza kupatikana madukani hivi karibuni.
Betri
Inakuja na betri la kukaa muda mrefu, kiwango cha betri lake ni mAh 3000, wakati simu ya iPhone 6S inakuja na betri la mAh 1,715 NA Galaxy S6 lina kiwango cha chaji cha mAh 2,550.
Pia inakuja na teknolojia nzuri ya kuchaji simu kuhakikisha utaweza kuchaji kutoka kiwango cha Sifuri hadi kufikia asilimia 50 ya chaji ndani ya nusu saa.
RAM
Uwezo wa RAM yake ni GB 3, hii ikiwa ni juu ukilinganisha na iPhone 6S inayokuja na GB 2 na inalingana na RAM ya Galaxy S6 yenye GB 3.
Inakuja na processor ya kisasa, ya 1.8GHz Snapdragon 808 hexa-core.
LUMIA 950 XL
Pia kufuata utamaduni wa Samsung na sasa hivi Apple pia, kampuni ya Microsoft imetoa toleo kubwa zaidi la simu hiyo kwa wanaopenda simu zenye umbo kubwa. Inaitwa Lumia 950 XL na inakuja na kioo cha inchi 5.7 ukilinganisha na cha inchi 5.2 ambacho Lumia 950 inakuja nacho.
Pia Lumia 950 XL inakuja na processor ya juu zaidi, ambayo ni 2GHz Snapdragon 810 huku sifa zingine zikifanana na za Lumia 950.
Simu hii itapatikana katika rangi mbili, nazo ni nyeusi na nyeupe. Lumia 950 itauzika kwa dola 549 za Kimarekani (Takribani Tsh 1,200,000/=) wakati kubwa yake itauzwa kwa dola 649 (Takribani Tsh 1,400,000/=).
Je umevutiwa na simu hizi? Kwa kiasi kikubwa TeknoKona tunaamini bado Microsoft ina nafasi ya kubwa ya kusumbua wengine katika biashara ya simu janja. Kwa kiasi kikubwa uzuri wa sifa za simu hizi na hii ikiwa ni pamoja na utumiaji wake wa programu endeshaji ya Windows 10 inaziweka katika nafasi nzuri katika kufanya vizuri sokoni. Tuambie maoni yako
No Comment! Be the first one.