Kampuni ya Microsoft wametambulisha rasmi tv mguso (touchscreen tv) ya inchi 84 ambayo itakubidi utoe si chini ya Tsh Milioni 40 (Dola elfu 20 za Kimarekani) kuweza kuipata. TV janja hii itakuwa inatumia toleo la Windows 10 na wenyewe wametengeneza wakifikiria utumiaji wa kiofisi zaidi ingawa inategemewa pia inaweza ikatumika katika mazingira mengine mbalimbali.
Lengo namba moja ni kwa TV hii kuweza kutumika kwa ajili ya kwenye vikao ambapo itaweza kutumika katika simu za video kupitia programu ya Skype. Pia watumiaji wataweza kuandika mambo mbalimbali kama vile ambapo wangeweza kutumia ubao n.k katika vikao. Badala ya ubao utaweza kuandika kwenye kioo cha TV hii kupitia apps zake mbalimbali zitakazokuwa katika toleo la Windows 10 linalotumika katika TV hiyo.
Kutakuwa na toleo la inchi 55 kwa ambao hawawezi kutoa pesa nyingi zaidi, toleo hili dogo litauzwa kwa takribani Tsh Milioni 14.
TV janja hii wataiita Microsoft Surface Hub
Sifa Spesheli
- Uweze wa kutumia Skype spesheli kwa wafanyabiashara, (Skype Business), ambayo itakuwa na uwezo kama vile kuwapigia simu washiriki wote wa mkutano watakaoshiriki kwa njia ya Skype.
- TV hii ina kamera zenye uwezo wa kutambua sura za watu waliokwenye eneo la mbele yake, kwa mfano wakati simu ya video inaendelea mtu anayetaka kuzungumza akiwa eneo la mbele la TV hiyo basi kamera zitaweza kujitaidi kumrekodi huyo anayezungumza zaidi.
- Undikaji kwa kutumia kioo cha TV hiyo, kama vile unapotumia tableti.
- Pia matoleo mapya ya apps za Windows kama vile Office, Powerpoint na zinginezo zilizokwenye vifaa vingine kama vile simu na tableti iwe ni Android, iOS n.k zitaweza kuwasiliana na TV hiyo kwa urahisi. Mfano uhamishaji wa faili ulilonalo kwenye simu kwenda kwenye TV hiyo kwa ajili ya kusomeka katika kikao n.k.
TV hii ya Surface Hub ina kamera mbili za kiwango cha HD kwa ajili ya kuweza kurekodi mbele (kwa watazamaji)
Hatua hii inazidi kuonesha uamuzi wa Microsoft wa kujaribu kufanya mambo mapya katika ubora mzuri zaidi ili kuhakikisha wanatengeneza njia mpya za mapato.
Je unadhani kununua TV ya shillingi milioni 20 ni sawa? Tueleze kwenye eneo la maoni, endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya Teknolojia!
No Comment! Be the first one.