Kampuni ya Microsoft hii leo wametambulisha tableti mpya (Surface Pro 3) yenye ukubwa zaidi wa upana na urefu kuliko matoleo ya nyuma. Surface Pro 3 inaupana wa inchi 12 kutoka 10.6, tableti hii wanaipa sifa ya kuwa na uwezo mkupya wa kushindana vikali na laptop katika uwezo wa ufanyaji kazi. Ikiwa na wembamba wa milimita 9.1 imekuwa ndiyo kompyuta/tableti nyembembe zaidi inayotumia ‘proccesor’ za Intel kuwahi kutengenezwa duniani.
Tokea Microsoft walete tableti ya kwanza ya Surface mwishoni wa mwaka 2012 bado hawajapata mafanikio makubwa kulinganisha na makampuni kama Apple kupitia iPads au Samsung kupitia Galaxy Tab. Kupitia toleo hili wanaendelea kufanya maboresho kwa kuzidi kuzipa uwezo mkubwa zaidi tableti zao. Surface Pro inakuja na Windows 8 na mtumiaji atakuwa na uwezo wa kutumia programu mbalimbali ambazo amezoea kutumia katika laptop au kompyuta ya kawaida ya Windows.
Katika kuwahakikishia wafanyabiashara na wafanyakazi kuwa Surface Pro ndiyo tableti iliyokikazi zaidi katika utambulisho wa tableti hii afisa Panos Panay wa Microsoft alisema, “Hii ndiyo tableti inayoweza kuondoa umuhimu wa kuwa na laptop”.
Surface Pro 3 Intel Core i3 inapatikana kwa bei ya dola za kimarekani 700 (Takribani Tsh 1,160,000) na kwa uwezo mkubwa zaidi bei inapanda zaidi.
Uwezo/Sifa
- Intel Core i3, i5 na i7
- Inakuja Peni ya kidigitali
- Kava lenye ‘Keyboard’ (Type Cover)
- USB Port
- Sehemu ya kuweka kadi ya diski (Card Reader)
Je Microsoft watafanikiwa katika kuongeza mauzo ya tableti zao? Muda utaonesha…
No Comment! Be the first one.