Hii ni habari mbaya kwa wapenzi wa Windows 10, Kwa haraka haraka ni kwamba Microsoft inawataka watu wahamie katika Windows 11.
Microsoft ni moja ya kampuni kubwa kabisa katika Nyanja ya teknolojia na ina bidhaa na huduma nyingi sana ambazo zinafanya kampuni kuwa moja kati ya kampuni kubwa kabisa duniani moja wapo ni Windows 10
Hapa inaongelewa Windows 10 Home and Windows 10 Pro ambazo zinauzwa katika mtandao wa Microsoft na jambo hili linategemewa kubadilika mpaka ifikapo januri 31 mwaka huu.
Naam hiyo ndio tarehe ya kusitisha huduma hiyo na baada ya hapo watu watalazimika kuhamia katika Windows 11.
Kumbuka programu endeshi ya Windows 10 imekua katika soko kwa kipindi cha zaidi ya miaka 7 na Windows 11 ilikuja kuingia sokoni mwaka 2021.
Cha kushangaza ni kwamba mpaka sasa Win 10 ndio inakua ni programu endeshi ambayo ina watumiaji wengi sana ukilinganisha na zingine zote.
Ukiachana na hayo yote kitu ambacho ni kizuri ni kwamba licha ya kuachana na kuuza leseni hizo kupitia mtandao kampuni bado itakua inatoa msaada wa kitaalam, ulinzi kwa win 10 mpaka kufikia mwezi oktoba mwaka 2025.
Pengine hiyo ndio tarehe ambayo wataachana kabisa na Win 10 kama walivyofanya kwa Windows XP n.k
Sasa basi kama utataka kushusha programu endeshi ya Win 10 ya kulipia huna budi kuingia katika mtandao wake kabla ya kampuni haijasitisha huduma hiyo.
kabla ya mwaka 2025 kuna hati hati kubwa kunaweza kukawa na toleo lingine la Windows ambalo litakua ni jipya na la juu kabisa ukiachana na toleo la Windows 11.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je hii umeipokea vipi? Je unadhani ni sahihi kwa Microsoft kuchukua hatua hii? Wewe itakuathiri vipi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.