Simu ya Lumia 650 inakuwa simu ya kwanza inayotumia toleo la Windows 10 na itakayouzika kwa bei nafuu ukilinganisha na matoleo mengine ya simu za Windows 10 kwa sasa.
Ingawa biashara ya simu haijaweza bado kuwa na mafanikio sana kimauzo na kimapato kwa Microsoft bado wanaonesha kuwa na nia ya kuendelea kuwa katika biashara hii.
Na sasa wamegundua njia ya kufanya hivyo ni pamoja na kupunguza idadi ya matoleo ya simu huku wakihakikisha matoleo machache wanayotoa yanagusa watumiaji wa aina mbalimbali na kwa uchaguzi wa bei za chini, kati na za juu. Simu ya Lumia 650 ni simu itakayoweza kutumia kwa matumizi ya kawaida na ata yale ya kikazi zaidi, na sifa kubwa ni kuwa itapatikana kwa bei nafuu zaidi ukilinganisha na zingine zinazotumia Windows 10.
Simu zingine za Windows 10 zilizokwisha tambulishwa na kuingia sokoni ni pamoja Lumia 950, Lumia 950 XL pamoja na Lumia 550.
Sifa za Simu ya Lumia 650
Muonekano
Inakuja na kioo (display) cha inchi 5 kikitumia teknolojia ya AMOLED – HD (720×1280). Imezungukwa na kijumba (body) cha alumini (alluminum).
Diski uhifadhi
Inakuja na kiasi cha diski uhifadhi (storage) cha GB 16 na uwezo wa kutumia memori kadi ya ukubwa wa hadi GB 200.
Prosesa na RAM
Inatumia prosesa ya ‘quad-core Qualcomm Snapdragon 212’ – 1.3GHz pamoja na RAM ya GB 1.
Kamera
Inatumia kamera yenye megapixel 8, ikiwa na uwezo wa ‘autofocus’ na flash ya LED.
Mengineyo
- Inakuja na kiwango cha betri cha mAh 2000
- Kutakuwa na toleo la laini moja na la laini mbili – ila hakutakuwa na tofauti ya sifa zingine katika simu hizo.
- Inakuja tayari na apps kadhaa muhimu kutoka familia ya apps za Microsoft. Hii ni pamoja na apps za Office (Word n.k), OneDrive na app ya Cortana.
Bei?
Simu hii itauzika kwa dola 199 za kimarekani kabla ya kodi n.k. Hii ni takribani Tsh 437,000/= | Ksh 20,270/=. Inategemewa kuongezeka kidogo ikianza kupatikana madukani hii ikiwa ni ongezeko la kodi na la faida ya wafanyabiashara.
Itaanza kupatikana kuanzia tarehe 18 mwezi wa pili kwa masoko ya Ulaya na kisha kusambazwa pia katika nchi zingine baada ya hapo.
Soma pia – Uchambuzi wa Microsoft Lumia 950 na Lumia 950 XL
Je unamaoni gani juu ya simu ya Lumia 650 na simu za Lumia kwa ujumla wake? Tuambie kupitia eneo la comment. Usisahau kusambaza makala kwa marafiki. Endelea kutembelea TeknoKona
Vyanzo: TheVerge na mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.