Kampuni la Microsoft kuanzia januari lilikuwa linafanya kazi ya kutengeneza keyboard katika vifaa vya iOs. Keyboard ambayo walikuwa wanaifanyia kazi ni ile maarufu katika simu za Windows ambayo inajulikana kama ‘Word Flow’
Mpaka sasa kampuni imeiweka keyboard hiyo kuweza kushusha lakini ikiwa katika toleo la majaribio (Beta). Toleo hili limewekwa makusudi kwa sababu kama watu watagundua matatizo katika keyboard hiyo wataweza kurekebisha. Mambo yote yakiwa sawa Word Flow katika iOs itaweza kauchiwa rasmi.
Word Flow inajumuisha vitu kibao kama vile Themes, sauti, na uwezo wa kuandika kwa kutumia mkono mmoja.
Kwa mtazamo wa kawaida keyboard hiyo inaonekana kama ni keyboard ya kawaida tuu tena ile iliyozoeleka kwa simu za iOS. Lakini jambo lake la kuweza kaundika kwa kutumia mkono mmoja linatofautisha kila kitu. Ukiwezesha uandishi wa kutumia mkono mmoja, maneno yatajipanga katika upande mmoja wa skrini.
Word Flow pia inaruhusu uandishi wa kawaida au ule wa kupitisha kidole juu ya maneno (swipe). Mara ya kwanza huduma hizi zilikua zinapatikana kwa App kama vile Swiftkey na Swipe.
Vipengele vya kawaida kama vile ‘Auto correction’ na kuotea maneno vinapatikana katika toleo hili. Bado mambo mengine ni kama vile theme za wakati wa giza na mwanga
Inavyosemekana kuna vipengele vingine kama vile kipengele cha kukuwezesha kufika kwa ukaribu katika taarifa zako za namba za simu. Pia kampuni ya Microsoft ina mpango wa kuongeza njia ya kufikia picha zako kwa urahisi hapo mbeleni.
Microsoft haikuweka wazi juu ya lini Word Flow itakuwa inapatikana katika na kuachiwa rasmi, kama nilivyosema kwa sasa lipo toleo la Beta tuu ambalo kama likipita basi kila mtu ataweza kujipakulia keyboard hii