Kwanza kampuni za Nokia Na Microsoft Ni makampuni mawili tofauti, wengi huchanganya hili. Wengi Tumezizoea kuziita Nokia Lumia, Sasa hiyo inabadilika. Wiki kadhaa zijazo jina La Nokia Lumia Litabadilika na simu hizo zitaitwa jina lingine. Kampuni ya Microsoft inayomilikiwa na Bill Gates imethibitisha kuwa haitatumia jina la Nokia katika simu za Lumia bali itatumia jina la “Microsoft Lumia”. Pia simu ya kwanza kwa Microsoft ambayo inabeba jina hilo inategemewa kutoka hivi karibuni.
“Ndio! Microsoft itaendelea kuuza simu zenye jina la Nokia, kama Nokia 130. Tuna leseni ya Nokia Kwa simu kama hizo” Alisema CMO, Tuula Rytilä wa simu za Microsoft
Haya mabadiliko yamekuwa ni ya kushangaza kidogo kwa sababu Microsoft ilipata biashara ya simu za Nokia kwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 7. Microsot ina haki ya kuuza simu kupitia jina la Nokia ndani ya miaka kumi kama makubaliano na leseni za mikataba yao inavyosema. Makubaliano hayo yanasemasema kuwa Microsoft iuze simu za S30 & S40 (symbian 3o & symbian 40) amabazo zinahusisha Simu-jinga (dumbphones) na simu za ‘Asha’. Simu zijazo za Lumia zimetoka nje ya leseni hii na haziwezi kuachiwa kuuzwa zikiwa na jina la Nokia. Majina ya ‘Asha’ Na ‘Lumia’ Yote yanamilikiwa na kampuni ya Microsoft
Microsoft imeshikilia namba 3 katika soko la Simu-janja nyuma ya Makumpuni makubwa ya Apple na Google. Tuambie wewe unaonaje mabadiliko haya hapo chini kwenye kiboksi sehemu ya comments.
Siku Njema!
No Comment! Be the first one.