Microsoft ni moja kati ya makampuni makubwa sana yanayojishughulisha na mambo ya teknolojia kwa ujumla.
Microsoft inamilikia App mbali mbali na Cortana ikiwa ni moja wapo, lakini kampuni imefikia muafaka wa kuachana na App ya cortana katika windows 11.
Cortana ni msaidizi wa dijiti (digital assistant) na kwa mara ya kwanza ilikua inatumika katika simu ambazo zilikua zinatumia windows na baadae kuhamia katika windows ya kompyuta.
Ikumbukwe pia miaka mitatu iliyopita Microsoft pia waliachana na App za Cortana kwa Androis na hata iOS.
Kwa sasa kama unatumia Windows 11 kama ukiingia katika cortana utakutana na ujumbe ambao unakuarifu ya kwamba imekataliwa na chini yake kutakua na link za kukufanya kujua zaidi kuhusiana na jambo hilo.
Vile vile Microsoft wanataka kuachana kabisa kutoa msaada wa kitalaam kwa watumiaji wa cortana kwenye Teams mobile, Microsoft Teams Display, na Microsoft Teams Rooms na hili litatokea kabla ya mwaka huu kuisha.
Haya yote yanatokea kwamba kampuni inaachana kabisa na App hiyo lakini cha kushangaza ni kwamba cortana ndani ya App ya Outlook katika simu bado itafanya kazi kama kawaida.
Ni ukweli usiopingika kwamba kwa miaka mingi sana Cortana imeshindana vita kali kutoka kwa huduma zingine kama vile Alexa au hata Google Assistant bila kufua dafu.
Japokua Cortana ndio imeachwa rasmi lakini Microsoft watakuja na App nyingine iitwayo Window Capilot ambayo itakua inafanya kazi zote za Cortana na zaidi.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni sawa kwa kampuni kuachana kabisa na Cortana?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.