Apple wanakuja kufanya mapinduzi ya hali ya juu kabisa katika teknolojia ya kompyuta kwa kuleta kifaa cha Vision Pro.
Vision Pro inatarajiwa kuingia katika soko hivi karibuni (matarajio februari 2) na makampuni mengi yamekua yakifanya juu chini ili kuhakikisha App zao zinapatikana humo
Kumbuka kifaa hiki kinatumia mfumo endeshi wa VisionOs hivyo basi App hizo zinatakiwa kufuata mfumo huo ili kupatikana katika App hiyo.
ZOOM na yenyewe imeweka wazi kwamba itaanza kupatikana katika kifaa hicho na mabadiliko ni mengi tuu ukinganisha na App ya kawaida mfano Android na iOS.
Kuna kipengele kinaitwa “Persona’ ndani ya mfumo mpya unaondana na VisionOS ambapo hapa watu wataweza kuonana katika mfumo wa Avatar za 3D ili kuonana na mtu
Unaweza ukaona mazingira yanayozunguka –kama vile uko katika mazingira hayo— kwa kipengele ambacho kinajulikana kama Spatial Zoom
Uwezo wa kutuma vitu na kuviona kwa karibua zaidi (kufanana na uhalisia) lakini vitu hivi vitakua katika mfumo wa 3D
Uwezo wa kuandaa mafaili, hotuba na kuweza kushirikisha watu au kuonyesha watu kwa kutumia kifaa hiki itawezekana n.k
Muelekeo ni mzuri na bado kuna App nyingi sana ambazo zinataka kuanza kupatikana katika vifaa vya Vison Pro.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je unadhani kifaa hichi kitaleta mapinduzi makubwa katika simu za mikutano?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.