Nchi ya Ethiopia imezuia mitandao ya kijamii katika kile ilichodai kwamba ni harakati za kuzuia wanafunzi wasisumbuliwe wakati wa mitihani ya mwisho wa mwaka ya kuingia chuo kikuu ambao unarudiwa wikii hii.
Mwezi uliopita mitihani hii ilifutwa baada ya maswali ya kwenye mtihani kuchapishwa katika mitandao ya kijamii ya Twitter, Facebook, viber na Instagram. Kwa mujibu wa mtandao wa News24 Mitihani hii inarudiwa wiki hii na kaitka kupambana na kuchapishwa kwa matokeo tena serikali ya Ethiopia imefungia mitandao ya kijamii toka siku ya jumamosi.
Soma Pia – Algeria yazuia mitandao ya kijamii kuzuia wizi wa mitihani
Ethiopia inakua ni nchi ya pili barani Afrika kufata hatua hii kupambana na wizi ama uvujaji wa mitihani kwa siku za hivi karibuni, Algeria ilizuia mitandao ya kijamii pia kwa sababu kama nizi wiki tatu zilizopita tena katika mitihani ya kuingia chuo kama hii.
Kumekuwa na mitazamo tofauti juu ya hatua hii na baadi ya wanaharakati wamepinga hatua hii kwa kusema kwamba sasa hivi ni hatua ya muda mfupi lakini inaweza ikatumika vibaya siku zinazokuja.
Hatua hii imekuja wakati ambapo baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa limepitisha suluhisho ambalo linapinga uzuiaji wa intanet kwamba ni ukiukaji wa haki za binadamu.
Wewe kama mdau wa intaneti hapa nyumbani unatuambiaje juu ya utaratibu huu wa kufungia mitandao ya kijamii kulinda uvujaji wa mitihani? tuambie katika maoni yako katika eneo la maoni nasi tutajibu.
Soma pia – Algeria yazuia mitandao ya kijamii kuzuia wizi wa mitihani