Katika hali ya kukabiliana na hali ya hewa chafu inayosababishwa na magari yanayotumia dizeli/petroli Uingereza nayo imeonekana kufuata nyayo za Ufaransa. Mwisho ni mwaka 2040 kwa magari yanayotumia mafuta huko Uingereza.
Moja kati ya vitu ambavyo vimekua vikiathiri mabadiliko ya tabia ya nchi duniani kote ni hewa chafu zinazozalishwa na viwanda, uchimbaji wa madini, n.k ikiwemo uchafu unazalishwa kwenye magari yanayotumia mafuta.
Magari mapya yanayotumia mafuta ya diseli na petroli nchini Uingezeza yataandolewa barabarani kuanzia mwaka 2040 kama njia ya kukabiliana na uchafuzi wa hewa.
Katika kuonyesha nia thabiti ya kukabiliana na hewa chafu itakonayo na magari yanayotumia mafuta Mawaziri watazindua ufadhili wa pauni milioni 255(zaidi ya $332 milioni) kusaidia kukabiliana na gesi chafu kutoka kwa magari yanayotumia dizeli ikiwa ni sehemu ya pauni bilioni 3 za kusaidia kusafisha hewa.
Ni wazi kwamba hatua hiyo itakuza sana mahitaji ya magari yanayotumia umeme na hivyo kufanya uhitaji wa magari hayo kuongezeka. Iwapo mtu bado atakuwa anahitaji kumiliki gari inayotumia mafuta basi atalipisha kiasi kikubwa cha fedha.