Kampuni ya Intel Corp imeomuondoa, Bw. Brian Krzanich kama mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo baada ya kubainika kuwa na mahusiano binafsi na mfanyakazi wa zamani wa Intel ikiwa ni ukiukwaji wa sera za kampuni hiyo.
Afisa mkuu wa fedha, Robert Swan ameteuliwa kushika nafasi ya Mkurugenzi mkuu wa muda wakati bodi inaendelea kutafuta mtu atakeyejaza nafasi hiyo, taarifa ya kampuni ilisema.
Krzanich mwenye umri wa miaka 58 alijiunga na Intel zaidi ya miongo mitatu iliyopita na mwaka 2013 akateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu huku jukumu kubwa lilikuwa ni kuipitisha katika kipindi cha ushindani mkali wa utengenezaji wa prosesa za kompyuta.
Bw. Brian Krzanich
Bw. Krzanich atakumbukwa kwa kuibakisha Intel katika ushindani kama mtengenezaji mkuu wa prosesa aliyejiunga na kampuni hiyo kama Mhandisi mwaka 1982.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
One Comment
Comments are closed.