Msichana mwenye umri wa miaka 18 nchini India aitwaye Uma Omram amefariki dunia kwa mlipuko uliosababishwa na simu ya Nokia 5233 wakati alipokuwa anaitumia kuongea.
Taarifa zinasema binti huyo alikuwa anaongea na simu hiyo iliyokuwa imechomekwa kwenye chaji ndipo mlipuko huo ulipotokea. Mlipuko huo ulimjeruhi mkono wake, mguu na kifua na baadae alikimbizwa hospitalini ambako ilithibitishwa kuwa ameshafariki.

Wakizungumzia tukio hilo kampuni ya HMD Global ambao ndio wazalishaji wa simu za Nokia walisema hawahusiki na simu hiyo kwa kuwa sio wazalishaji kwa kipindi simu hiyo inatolewa.
Kampuni ya HMD Global ilinunua jina la Nokia kuanzia Desemba 2016 na haijulikani nani atawajibika kwa tukio la binti huyo. Wamiliki wa Nokia wanasema ingawa hawawezi kuthibitisha tukio hilo lakini pia wanadai hawawajibiki kutokana na tukio hilo kwani simu hiyo haikuuzwa chini ya kampuni yao.