Motorola ni moja kati ya chapa maarufu sana zinazotengeneza simu janja, toleo lake la RAZR ni moja katika ya matoleo yanayoiwakilisha vyema kampuni.
Kwa sasa kampuni hiyo iko katika hatua za kutengeneza matoleo mengine mawili ya simu za RAZR ambayo yatatoka 2023
![Motorola RAZR](https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/uploads/2022/07/Moto-Razr-2022.webp)
Ukifikiria sana utagundua kuwa matoleo hayo yatakua ni mshindani mzuri kwa kampuni ya Samsung na simu janja zake za Samsung Fold.
RAZR ya kwanza licha ya kuiwakilisha kampuni vizuri katika soko ila kuna vitu vilikua haviko sawa (kwa wakati ule) maana ni simu mpya lakini ilikua ina sifa ambazo haziendani kwa mfano ilikua na 16MP katika kamera
![Motorola RAZR 2022](https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/uploads/2022/10/Motorola-RAZR-2022.jpeg)
Kingine ni kwamba ilikua na uwezo mdogo wa betri yaani 2,500mAh na vile vile simu hii ilikua ni gharama sana, wakati kwa bei hiyo ungeweza pata simu janja yenye sifa nzuri zaidi.
Ni wazi kuwa baada ya hii kampuni pia iliachia simu nyingine katika muendelezo wa matoleo ya RAZR lakini bado ilikua ni bei ghali ukilinganisha na simu ya Samsung Galaxy Z Flip 4.
Pingine kwa sasa hii haitakua ni sababu, lakini bado vile vile sifa za ndani za simu janja hizi mpya hazijawekwa wazi hivyo haiwezekani kuzizungumzia kwa undani.
Hapa kilio cha wengi ni kwamba kampuni inabidi itafute namna ya kupunguza bei ya kifaa hicho kikiwa sokoni maana mifano kwa matoleo yalipita wanayo.
![Motorola RAZR Ya Mwaka 2022](https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/uploads/2022/10/Motorola-RAZR-Ya-Mwaka-2022.webp)
Ni wazi kuwa kuna makampuni mengi sasa yamejitoa kabisa ili kupambana na Samsung, ukimtoa Motorola kuna Oppo nae anaandaa simu matata za kupambana nazo katika soko la simu janja (za kujikunja/kujipindua)
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je umeshaanza kutumia huduma hii? Kama bado je uko tayari?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.