Motorola inajiandaa kuzindua simu mpya mbili za Moto G mnamo Septemba. Moto G84 5G na Moto G54 5G zitakuwa nyongeza za hivi punde kwa safu maarufu ya Moto G ya Motorola.
Motorola wamesema simu zote zinakuja na uwezo wa kudumu na chaji kwa siku mbili kwa matumizi ya kawaida. Simu zote zinauwezo wa kuchaji haraka (fast charge), Moto G54 5G ikija na betri la mAh 6,000 na uwezo wa kuchaji wa 18W wakati ile ya G84 5G ikija na betri la mAh 5,000 na teknolojia ya kuchaji kwa haraka ya kiwango cha 33W.
Simu zote mbili zinatarajiwa kuja na programu endeshaji ya Android toleo la 13 huku ikiwa na uwezo wa kupokea sasisho la Android 14. Pia zinatarajiwa kuanza kupatikana nchini India na masoko mengine kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.
Hii hapa jedwali linalolinganisha sifa za simu hizi mbili:
Kipengele | Moto G84 5G | Moto G54 5G |
Skrini | pOLED ya inchi 6.5, 120Hz | IPS LCD ya inchi 6.5 |
Processor | Qualcomm SM6375 Snapdragon 695 5G |
MediaTek Dimensity 7020 SoC
|
RAM | GB 12 | GB 8 au GB 12 |
Uhifadhi | GB 256 | Toleo la RAM ya GB 8 linakuja na uhifadhi wa GB128, RAM 12 linakuja na GB 256 |
Kamera za nyuma | 50MP kuu, 8MP ultrawide |
50MP kuu, 8MP ultrawide
|
Kamera ya mbele | 16MP | 16MP |
Betri | 5000mAh | 6000mAh |
Mfumo wa uendeshaji | Android 13 | Android 13 |
Moto G84 5G inatarajiwa kugharimu karibu $300 (TZS 660,000), wakati Moto G54 5G inatarajiwa kugharimu karibu $250 (TZS 550,000).
Ingawa simu hizi zinaweza kuonekana zinafanana sana kuna tofauti chache kuu;
- Kwenye kamera, kamera ya ultrawide ya Moto G84 5G inakuja na teknolojia bora ya ‘autofocus’ wakati hii inakosekana kwenye G54 5G, tofauti hii inafanya picha za Moto G84 5G kuwa na muonekano bora zaidi ata kwa picha za eneo lisilokuwa na mwanga wa kutosha.
- Tofauti nyingine kubwa ni kwenye teknolojia za skrini zake, Moto G84 5G inakuja na teknolojia ya pOLED. Teknolojia hii inamuonesho mzuri zaidi wa picha na video kuliko wa skrini za IPS LCD. Rangi zitaonekana kwa ubora zaidi kwenye pOLED ukilinganisha na za IPS LCD.
Simu zote mbili ni chaguo zuri kwa wale wanaotafuta simu mpya ya hadhi ya kati au ya bajeti ya wastani. Moto G84 5G inakuja na prosesa yenye nguvu zaidi na mfumo bora zaidi wa kamera, wakati Moto G54 5G ni nafuu zaidi ingawa kwenye diski uhifadhi wa GB 64 inaweza ikawa wameinyima sana.
Simu ipi kati ya hizi imekuvutia zaidi?
Vyanzo:Phonearena na vingine mbalimbali
No Comment! Be the first one.