Ukiwa unaperuzi kwenye Twitter ukaona akaunti ikiwa na alama ya pata kwa pembeni upande wa kulia hakika mtu huyo atakuwa ana kitu cha ziada ambacho kimemfanya aweze kuwekewa alama ya kipekee ishara ya kwamba ameidhinishwa!.
Kila siku Twitter inaidhisha akaunti za watu lakini kuna taarifa kuwa mtandao huo wa kijamii upo kwenye hatua za mwisho katika kuleta mchakato mpya ambao unahusisha hatua mbalimbali ambazo itakuwa ni LAZIMA kwa yeyote atakayeomba akaunti yake itambulike kwa namna ya kipekee.
Je, mtu yeyote anaweza kuomba akaunti yake ya Twitter iidhinishwe?
Jibu ni ndio lakini lazima iwepo sababu maalum ya kwanini Twitter waiwekee alama ya kipekee mathalani unaweza kuwa mtu maarufu (mwanamuziki, mwanamichezo, n.k), serikali, mwanaharakati na si hivyo tuu bali ni lazima wahusika wajiridhishe kuwa unastahili kupewa kile ulichoomba kulingana na vigezo walivyoviweka.
Katika mpango huu mpya Twitter inafanyia kazi kile ambacho ilisitisha mwaka 2017 ukihusisha mchakato wa maombi ya akaunti kuidhinishwa ambapo mhusika atatakiwa kujibu maswali kipengele baada ya kipengele kabla ya kuyatuma kwenda kwa wahusika kwa ajili ya kupitia na hatimae kukubali ama kukataa kilicholetwa mbele yao.
Kuhusu lini tutaanza kuyaona maboresho hayo mapya (kuidhinisha akaunti) haijulikani lakini taarifa zainasema Twitter wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha suala hilo.
Vyanzo: Twitter, Gadgets 360
One Comment