Telegram ni moja ya mitandao ya kijamii mikubwa sana na ina sifa ya kuwa na vipengele vingi sana ukiachana na sifa yake ya kuwa na ulinzi na usalama wa hali ya juu.
Mara kwa mara kampuni imekua ikijihakikishia inatoa masasisho (update) yenye tija sana kwa watumiaji wake.
Sasa wanakuja na masashisho kadhaa lakini kubwa katika hayo ni uwezo wa kuweza kujiunga katika mtandao huo bila hata ya kutumia namba yako ya simu, kitu ambacho mwanzoni kilikua hakiwezekani.
Yaaani Telegram ili kujiunga ilikubidi uweke namba ya simu kama unavyofanya wakati unaanza kutumia mtandao wa WhatsApp.
Lakini vile vile ikumbukwe katika mtandao wa telegram namba za simu zilikua hazionyeshwi kwa watu ambao huwajui yaaani hapa mtumiaji….
….. alikua na uwezo wa kuruhusu/kukubali nani aweze kumpata kwa kutumia namba yake ya simu – kwa kifupi ni maamuzi ya mwenye akaunti.
Kwa sasa hilo mtandao umelipiga chini na upo katika kujikita zaidi katika swala la kuilinda faragha (privacy) na kinachofanyika hapa…..
….. ni kwamba utakua na uwezo wa kuingia katika mtandao huo kwa kutumia namba ambazo hazijulikani na zitakua zimezalishwa na mfumo mzima ambao unamilikiwa na telegram wenyewe (hutatumia namba yako ya simu).
Sasisho lingine ndani ya mtandao huu ni uwezo wa kuweka muda wa meseji kujifuta wenyewe. Kwa wale watumiaji wa mtandao wa WhatsApp jambo hili sio geni sio?
Kinachofanyika hapa ni kwamba kipengele hiki hakiwezi kufanya kazi kwa meseji za nyumba –kabla ya kipengele—bali za mbele tuu na uzuri wake ni kwamba wewe ndio unapanda muda wa meseji kufutika.
Vile vile ukiachana na mambo hayo bado mtandao umetoa masasisho mengine mengi lakini yote yanajikita katika swala zima la kuboresha ulinzi na usalama bila ya kusahau faragha.
Kwa mfano kama mtumiaji wa App hana jina tambulishi (User name) ana uwezo wa kutengeneza QR code ya muda na ku’share na watu katika mitandao mingine ya kijamii.
Ili kufurahia yote haya hakikisha una toleo jipya kabisa la mtandao huu wa Telegram.
Ningepa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani vipengele hivi vipya vina tija kwako?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.