Mradi mkubwa kuliko yote duniani wa nishati ya Jua ni ule wa Mohammed bin Rashid Al Maktoum uliopo kwenye nchi za falme za Kiarabu (UAE). Mradi huu ulianza rasmi mwezi Oktoba mwaka 2013 na ulikuwa chini ya usimamizi wa Mamlaka ya umeme na maji Dubai (DEWA). Mradi huu umechukua nafasi ya kilomita za mraba 77 na upo kilomita 50 kutoka mji wa Dubai.
Katika mradi huu kuna aina mbili tofauti za paneli za sola zinazotumika ambazo ni Photovoltaics (PV) pamoja na Concentrated Solar Power (CSP). Mpaka sasa ujenzi wa mradi huu umefikia awamu ya 5 ambapo awamu ya 4 na 5 bado zinaendelea kutengenezwa. Awamu ya kwanza mpaka ya tatu zimeshakamilika na zinatumika sasa hivi kuzalisha umeme Emirates.
Awamu ya kwanza ya mradi huu ilihusu uzalishaji wa Megawati 13 (13MW) kwa kutumia paneli za Photovoltaic. Mpaka kukamilika kwa awamu hii zilitumika paneli 152000 na transfoma 13 za kuchuja umeme. Awamu hii ilifanikiwa kuzalisha kilowati milioni 28 kwa lisaa (28kWh).
Awamu ya pili ya mradi huu ilihusu kuzalisha Megawati 200 (200MW) na ulianza kujengwa rasmi mwaka 2017. Mradi huu wa awamu ya pili ulitumia jumla ya paneli za sola milioni 2.3 na ulisambaa katika eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 4.5.

Awamu ya tatu ya mradi huu ilihusu uzalishaji wa Megawati 800 (800MW) ambapo mamlaka ya umeme na maji Dubai (DEWA) ikishirikiana na makampuni mbalimbali ilianza ujenzi wa mradi huu mwaka 2018.
Awamu ya nne inahusu uzalishaji wa Megawati 950 (950MW) na ile ya tano inahusu uzalishaji wa Megawati 900 (900MW). Mpaka kufikia mwaka 2030 miradi yote hii itakuwa imeshakamilika na kuanza kutumika. Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu tembelea tovuti hii.
No Comment! Be the first one.