Msanii Soulja Boy wa nchini Marekani ameingia mkataba na kampuni moja ya elektroniki na kufanikiwa kuingiza sokoni kompyuta za tableti zenye jina lake wiki hii.
Kampuni hiyo inafahamika kwa jina la Tokova na msanii huyo wameingia mkataba ambapo msanii huyo alihusishwa kwenye ubunifu wa tableti hiyo iliyobeba jina lake.
Tableti hizo zinatumia programu ya Android na ni toleo la Ice Cream Sandwitch, zinaitwa Tokova Soulja Boy Edition na zitakuwa jina pamoja na picha ya msanii huyo. Kutakuwa na matoleo mawili, moja la ukubwa wa inchi 7 na jingine inchi 9.5, kila moja ina uwezo wa kuhifadhi data wa GB 64, pamoja na RAM ya GB 2.
Kwa bei ya ukubwa inchi 7 inauza dola za kimarekani 400 ( takribani Tsh 632,000/=) wakati ile kubwa zaidi ya inchi 9.5 itauzwa dola 500 (takribani Tsh 790,000/=). Bei hii ipo juu sana ukilinganisha na tableti nyingine za Android lakini watafiti wanatabiri itauzika tuu kwani kwa mashabiki wake kumiliki tableti hii litakuwa jambo la furaha.
Msanii huyu kawa wa kwanza kufanya jambo hili, je ni nani atafuata? Kwa bongo yetu mnaonaje mtu kama Fid Q na wengine waanze kuporomoka na Simu au Tableti za majina yao? Je, utanunua ya nani?
No Comment! Be the first one.