Kwa mujibu wa ripoti mpya watumiaji wa WhatsApp duniani kote tukiangazia muda wa jumla inaelezwa walitumia saa bilioni 85 kwenye programu hiyo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Ripoti hiyo ambayo imeenda mbali zaidi na kubainisha kuwa kila mtu anatumiwa wastani wa saa 11. 425 na takwimu zinaonyesha WhatsApp ina watumiaji karibu bilioni 1.5.
Saa 30 bilioni zimetumia kuperuzi mtandao wa kijamii wa Facebook.
Kwa upande michezo (Games) iliyochukua saa nyingi kuchezwa ni My Talking Tom, Candy Crush Saga, Fortnite, Lords Mobile, Subway Surfers, Helix Jump, Slither.io, PUBG Mobile na Fishdom.
Michezo hiyo kwa jumla ilitumia saa bilioni 3.83 kujifurahisha kupitia watumiaji wa simu duniani.
Ripoti ya utafiti inaonyesha watu wa Marekani wanatumia angalau saa tatu na nusu kwa siku kutumia simu.
Progamu 10 ambazo zinatumiwa zaidi ni WhatsApp, WeChat, Facebook, Messenger, Pandora, YouTube, Instagram, Twitter, Google Maps, na Spotify.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.