Muonekano mpya wa Instagram waja rasmi. Tuliandika hivi karibuni kuhusu Instagram kuja na muonekano tofauti, jambo hilo sasa ni rasmi na huu ndio muonekano wake mpya.
Walichojitahidi Instagram ni kutoacha historia yao kuu katika muonekano wao mpya. Kutokana na mabadiliko makuu ya mfumo wa muonekano katika Apple, yaani iPhone na iPad, pamoja na Android na ujio wake wa Material Design…moja kwa moja app ya muonekano wa app ya Instagram ukaanza kuonekana kutofanana vizuri na programu endeshaji hizo.
Kuanzia kwenye ‘icon/logo’, yaani alama kuu mabadiliko yamefanyika. Angalia picha hii chini.

Mabadiliko ya kimuonekano wa ndani ya app ipo kama hivi…kushoto ni muonekano wa zamani na kulia ni wa sasa.

App ya Instagram ni moja ya app muhimu sana kwa familia ya apps zinazomilikiwa na kampuni ya Facebook. Kwa sasa app ya Instagram inawatumiaji takribani milioni 400 na watumiaji hawa wanaupload video na picha takribani milioni 80 kila siku.