Licha ya baadhi ambayo kampuni ya Huawei imewekewa lakini bado siku hadi siku inazidi kuwashangaza watu maana hawapoi!
Huawei ni moja kati ya makampuni makubwa kabisa katika maswala mazima ya teknolojia na ni wazi kuwa wana vitu vingi sana chini yao na kimojawapo ni utengenezaji na uuzaji wa simu janja.
Fununu zilikua zikizagaa katika mtandao kwa muda mrefu sana kwamba kampuni hiyo inataka kuachia simu janja mbili ambazo zitashindana katika soko.
Simu hizo ni muendelezo wa matoleo ya P60 ambayo itakua imejikita sana katika maswala ya picha/video na toleo jipya katika matoleo ya Mate 60.
Ni wazi kwamba simu hizi mbili zitakuja na sifa za undani za aina yake na zitakua ni simu shindani na zile ambazo ziko sokoni kwa wakati huo.Ukiachana na teknolojia nyingi ambazo kampuni inazo kwa sasa wanaamua kuja katika soko la simu na bidhaa hizi mbili kwanza
Muonekano wa P60 ambao umesambaa mtandaoni unaonyesha simu hiyo ina kamera kubwa huku umbo lake likiwa zuri, kioo kikubwa ambacho kinafika mpaka pembezoni kabisa mwa kuta za simu hizo.
Ma muonekano wake wa haraka haraka ni kama yale matoleo ya Samsung Edge katika upande wa mbele, kumbuka teknolojia hii simu nyingi kwa sasa hazitumii kama zamani.
Sifa zingine za undani haziko wazi, lakini tutakujuza mara tuu tukizipata maana fununu zinasema kuwa simu hizi zinatambulishwa rasmi sokoni mwezi wa tatu mwaka huu.
Ni wazi kuwa lazima kutakua na maboresho kadha wa kadha kulinganisha na matoleo yake ya nyuma –ya simu hizi– maana huu ni sehemu tuu ya muendelezo wa matoleo hayo.
Je ni mtumiaji wa Huawei? Hili umelipokeaje? Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment unaweza ukaanza kutumia simu hizi kutoka kwao?.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.