Samsung imekua ni moja kati ya kampuni ambalo linaingiza vifaa vya aina yake katika soko, katika siku za hivi karibuni kumekua na picha kadha za Galaxy S23 zikiwa zinasaambaa katika mtandao.
Picah hizo zilitufunza machache kuhusiana na kifaa hicho kipya ambacho bado hakijaingia sokoni, tulipata taarifa kama vile za aina ya rangi katika vifaa vyote hivyo vine—ndio zinakuja zikiwa katika rangi nne!
Rangi hizo ni: Nyeusi, kijani, pinki na ‘baige’ ambazo kama ni mfuatiliaji mzuri wa matoleo ya simu utagundua kwamba rangi hizo sio ngeni sana katika simu mbalimbali.
Kingine ni kwamba picha hizo zimeonyesha kuwa mateleo ya simu hizi hayatakua na umbo tambarale kama simu nyingi za sasa katika kona zake.
Hapa Samsung wanabadilika kidogo maana toleo la S23 litakua na ‘kona ya kubembleza’ kama vile matoleo yake ya zamani ya S yalivyokua.
Finally seeing some new colors on the S23 Series, although much lower volume than the main 4 colors. The new colors on the S23 Ultra include Gray, Light Blue, Light Green and Red in addition to Beige, Black, Green and Light Pink.
— Ross Young (@DSCCRoss) January 6, 2023
S23 ina uwanja mkubwa sana katika sehemu ya kioo na pia vile vile imetengenezwa katika mfumo ambao inakua ni rahisi katika kuishika.
Kamera yake ya mbele inakua ipo ndani kabisa ya kioo – simu janja nyingi siku hizi zinatoka zikiwa na teknolojia hii.
Vitufe vya sauti viko katika upande wa kulia, pia hata cha kuzima simu upande huo huo. Sehemu ya kupitisha chaji iko chini huku ikiwa na tundu la USB Type-C.
Ukiachana na muonekano huo kuvuja katika mtandao lakini hakuna chochote kilichovuja katika swala zima la sifa za undani wa Samsung Galaxy S23.
Pengine mpaka siku ya uzinduzi (februari 2023) wa kifaa hiki ndio watu watapata kujua sifa za undani kabisa na kifaa hichi na hata bei pia
Ningependa kusikia kutoka kwako niandikie hapo chini katika eneo la comment, je simu hii ikitoka utapenda kutumia rangi gani katika hayo machaguo manne?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.