Windows 11 ni programu endeshi ambayo inawika sehemu nyingi duniani na inachagizwa na upya wake kitu ambacho watu wengi ulimwenguni wanaweka toleo hilo kwenye kompyuta zao bila kujali kifaa husika kimekidhi vigezo vya kuwa na sifa zinazohitajika kuwa katika sehemu salama ya kupakua masasisho yanapotoka.
Maboresho mbalimbali yamekuwa yakifanyika kwenye toleo hilo la programu endeshi tangu kutoka kwake rasmi mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana, Bado tutazidi kuyafahamu mengi lakini hivi sasa umetoka muundo mpya wa mpangilio wa vitukwenye ile sura ya tabiti kwenye Windows 11.
Katika maboresho ambayo yameletwa ni uwezo wa kuchaguakuonekana kwa vitu vingi au vichache kifaa kikiwa katika muundo wa muonekano wa tabiti; ule mstari wa chini kabisa kwenye sura ya mbele ya Windows 11 hivi sasa mtumiaji watoleo husika la programu endeshi anaweza kupanga vikaonekana vitu vichache tu mfano alama ya Bluetooth, intaneti (WiFi), n.k.
Pia, katika muonekano huo wa tabiti kwenye Windows 11 inaonekana vionjo viongezeka hasa katika muonekano ambapo sasa mtu anaweza kubofya sehemu na kuona vitu vingi ambavyo vinakuwa na maelezo kuhusu habari fulani.
Halikadhalika, maboesho hayo yamekwenda sambamba na ujio wa vikatuni vipya ambavyo mtu anaweza kuvitumia kumaanisha kitu fulani katika mtindo wa lugha ya picha.
Tukumbuke kuwa ili kuweza kuona maboresho hayo (mathalani muonekano wa tabiti kwenye Windows 11) ni lazima kuyapakua na daima ni muhimu kwani pamoja na mengineyo yanayoboreshwa ni kwa ajili ya kufanya kompyuta zetu ziwe na ulinzi madhubuti.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.