SpaceX inatazamiwa kufanya safari yake ya kwanza kwenda kwenye Mwezi miaka michache ijayo na kampuni hiyo imekuwa ikifanyia maboresho chombo husika ili kuwa safari ya kihistoria na yenye mafanikio. Sasa wamezindua muundo mpya wa roketi hiyo.
Safari hiyo ya mwaka 2023 ambayo tayari imeshapata mteja wa kwanza ambapo maandalizi ya kufanikisha safari hiyo yameonekana kuendelea vyema huku muundo huo mpya wa roketi inayoitwa Big Falcon Spaceship ukivutia.

Pata kufahamu undani wa roketi itakayowapeleka watu kwenye Mwezi.
Urefu na idadi ya watu inayoweza kubeba. Roketi yenyewe kwa mujibu wa Bw. Elon Musk ina urefu wa futi 387 yenye uwezo wa kubeba abiria mpaka mia moja (100) pamoja na mizigo.
Unguvu (Ufanisi wake). Chombo hicho kinaelewza kuwa na injini takribani thelathini na moja ambazo zina nguvu ya tani 5400 kwa pamoja.

Safari yenyewe. Mwaka 2023 ndio mwaka rasmi ambao safari hiyo itaanza ingawa inaweza kuwa mapema zaidi na si tu kwamba itakuwa ni kufika kwenye mwezi pekee bali kifaa hicho kitafika mpaka kwenye sayari ya nne (Mars) na watalii kuweza kuona vitu ambavyo tumevisoma kwa nadharia.
Majaribio. Hakuna sayansi inayofanyika bila kujaribu kwanza kabla ya kuanza kutumika rasmi; roketi iliyotengenezwa na SpaceX na itakayofanya safari ya kwenda kwenye Mwezi pamoja na sayari ya nne itazamiwa kuanza kufanyiwa majaribio mwaka 2019 mwushoni bila kuwa na watu ndani.
Matarajio ni ni kwenda mpaka kwenye “Sayari Nyekundu” mwanzoni mwa mwaka 2024 huku safari ikitazamiwa kuanza mwaka 2022-23.
Vyanzo: The Verge, Mashable