Kwanza ningependa kutanguliza shukrani kwa wasomaji wetu, bila nyinyi TeknoKona isingeendelea kuwa hapa. Tunayofuraha kuwataarifu ya kwamba mwanzilishi wa TeknoKona, Stephen Mokiwa kwa jina jingine KijanaMokiwa…. Nimefanikiwa kuingia katika kuwania tuzo zinazofahamika kwa jina la TAYPA – Tanzania Annual Young Professionals Awards.
Katika tuzo hizo nipo kwenye kipengere cha ‘Pioneer’, hili ni neno la kiingereza linalomaanisha mtu aliyejikita katika kufanya kitu cha kitofauti kabla ya wengine. Kupitia uanzishwaji wa TeknoKona na lengo likiwa ni kutoa habari na maujanja ya yahusuyo teknolojia katika lugha kiswahili tokea mwaka 2012 watu wengi zaidi wameweza kujifunza na kupata habari kwa haraka na katika lugha yetu inayoeleweka zaidi.
Ungana nami katika kuhakikisha ushindi katika tuzo hii unapatikana. Ushindi hautakuwa wakwangu bali ni wa jumuiya nzima ya waandishi na wasomaji wa TeknoKona.com!
Kunipigia kura andika D1 tuma kwenda namba 15678, gharama ni za sms za kawaida. Hii ikimaanisha ni za nje ya vifurushi na hivyo unatakiwa uwe na vocha kwenye simu yako. Na unaweza kunipigia mara nyingi uwezavyo. Asante sana!
No Comment! Be the first one.