TikTok inamilikiwa na kampuni ya china inayojilikana kama ByteDance, licha ya kampuni hii kujipatia mapato na umaarufu mkubwa kupitia TikTok bado uwekezaji unaendelea.
Kwa sasa wanajikita katika uwekezeaji katika teknolojia ya Virtual Reality (VR) –kwa haraka haraka unaweza ukasema ni uhalisia ambao unatengenezwa na teknolojia.
Kwa sasa kampuni ipo katika hatua za kuajiri watu na inasemekana kuwa kuna Zaidi ya ajira 40 kuhusiana na teknonolojia hii.
Mwaka jana ByteDance walinunua Pico, ambayo ni kampuni inayojihusisha na mambo ya Virtual Reality (VR).
Hizo nafasi za kazi Zaidi ya 40, ni kwa ajili ya kampuni ya Pico na san asana ni kwa ajili ya huko California na Washington.
Kampuni ya Pico licha ya kuwa inamilikiwa na kampuni kubwa sana ni kwamba bado ina kazi kubwa katika kuhakikisha kuwa inakua kwa kiasi kikubwa.
CHANZO: Protocol
Ningependa kusikia kutoka kwako niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unahisi kuwa VR ni teknolojia ya kuzingatiwa sana na ByteDance?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.