Mtandao wa kijamii wa Twitter ushajijengea sifa ya kuwa moja ya eneo muhimu la kuwa na ushiriki kwa watu na makundi mbalimbali kwa nia ya kusambaza taarifa mpya pamoja na kushiriki katika mazungumzo. Ila ubaya ni mmoja si kila mtu au kundi anaweza akaruhusiwa kuendesha akaunti katika mtandao huu maarufu.
Mtu au kundi lolote lenye kutoa vitisho au vurugu za aina yeyote basi hujikuta katika hali ya kufungiwa akaunti hiyo, na kutokana na hali hii makundi yote yanayotambulika kuwa ya kigaidi huwa yanafungiwa akaunti mara moja baada ya kugundulika. Na hapa ndipo utata na kundi linalosemekana kuwa la kigaidi la ISIS linapokuja.
Kundi hilo limetoa kitisho cha kumuua Bwana Jack na wafanyakazi wa mtandao huo kutokana na hali ya kufungiwa akaunti kila wanapofungua akaunti mpya kwenye mtandao huo maarufu.
Twitter imesema inashirikiana na vyombo vya usalama kujua hatua zaidi za kuchukua kutokana na kitisho hicho.
No Comment! Be the first one.