Moja kati ya maswali ambayo watu wengi wanajiuliza, je WhatsApp wanapata faida? Maana huduma ni ya bure na pia kampuni hiyo ilinunuliwa kwa gharama kubwa na Facebook, huku hakuna matangazo yoyote yanawekwa kwenye WhatsApp kama ilivyo kwenye mitandao kama Facebook, Instagram n.k
Mimi na wewe tunabaki kuwa na lundo la maswali kichwani bila majibu, leo hii mitandao ya kijamii inapata faida kubwa kutokana na wingi wa matangazo lakini kuna Whatsapp ambayo imekuwa sehemu ya maisha yetu na inajiendesha bila ya matangazo wala haina gharama za kujiunga na ina watumiaji zaidi ya billion 2 Duniani.
Nikupe historia fupi kidogo, Whatsapp iligunduliwa mwaka 2009 na vijana wawili waliokuwa wakifanya kazi Yahoo! , Brian Acton na Jan Koum. kwa wale walioanza Kutumia Whatsapp zamani unakumbuka ulikuwa unalipia $1 kwa mwaka.
Mwaka 2014 ilinunuliwa na Facebook kwa gharama ya $19 billion za kimarekani, na baada ya hapo wakasitisha huduma za malipo watu wakaanza kupakua bure na kuzidi kufurahia maisha.
NJIA ZINAZOINGIZA PESA WHATSAPP
Licha ya kuwa Whatsapp unaitumia bure lakini kuna njia kuu mbili zinazoingiza Pesa.
1. Whatsapp For Business
Inajulikana kama “Whatsapp business”, wengi mnaitumia bure lakini kuna namna inaingiza Pesa ya kutosha.
Mwaka 2018 Whatsapp walitengeneza App inayojitegemea maalumu kwa ajili ya Biashara, iliitwa Whatsapp business, mtumiaji anaweza kutengeneza Whatsapp account na ikawa verified, anaweza kuweka website links, kuunganisha na social media kupitia Whatsapp business n.k
Unaweza kuunganisha biashara tofauti tofauti kupitia Whatsapp business, hivyo unaweza kuwatumia wateja wako jumbe (notifications) kuhusu huduma zako na wao wakajibu, Lakini mwenye biashara/kampuni ukijibu ujumbe wa mteja baada ya masaa 24 kupita utatozwa gharama kwenye kila ujumbe unaotuma, hiyo ni njia mojawapo ya kuingiza faida.
2. Kuunganisha na kubadilishana taarifa kati ya WhatsApp na Facebook (Facebook Connection)
Kama ulikuwa hujui Facebook wanatumia kipengele cha kubadilishana/ku-share matangazo kutoka Facebook kwenda WhatsApp na kinyume chake. unapo-share tangazo kutoka Facebook kwenda Whatsapp ujue wao wameingiza pesa, ni kama unawasaidia kutangaza ili tangazo liwafikie wengi zaidi.
Facebook pia wanatumia taarifa za WhatsApp kama namba ya simu ili kuweka mazingira mazuri wa kuonyesha matangazo kulingana na sehemu husika mtu alipo.
Hizo ni njia kuu mbili ambazo WhatsApp inapata Faida, usione kitu/App unatumia bure ukafikiri haingizi faida, wanapata hela nzuri kuputia watumiaji, kuna msemo unasema “If you dont pay for the product then you are the product” yaani “kama unatumia kitu flani bila kulipia basi wewe ndiyo bidhaa”
No Comment! Be the first one.