Usalama kwenye maisha yaliyotawaliwa na teknolojia ni kitu muhimu sana hasa pale unapopenda kuwa mtu wa kutopenda kuweka mambo yako wazi na katika zama hizi za kidijitali matumizi ya nenosiri si jambo la ajabu.
Katika maisha ya kwenda na teknolojia siku hizi ni mara chache mtu kutumia kalamu na karatasi kuandika nyaraka na badala yake kompyuta kupitia programu wezeshi imekuwa ikifanya kazi hiyo. Sawa, umeandika barua yako lakini suala linakuja pale ambapo unataka kuweka ulinzi ili kwa mtu yeyote atakayetaka kuifungua basi akutane na kizingiti. Je, utafanyaje?
Jinsi ya kufunga nyaraka kwenye Ms. Word 2010/2013
Kwanza kabisa ni kufungua programu husika (Microsoft Word 2010) kisha unaanza kuandika unayoyataka kuyaweka kimaandishi na baada ya hapo inafuata hatua ya kutunza nyaraka kwa lengo la kuweza kuipata kiurahisi pale utakapoihitaji kwa mara nyingine tena. Sasa mara bada ya hilo kukamilika tutazame ukurasa wa pili: Namna ya kuifunga nyaraka kwa nywila.
- Ndani ya Ms. Word nenda kwenye File > Info > Protect Document > Encrypt with Password,
- Weka nenosiri (nywila) unalotaka kisha bofya OK,
- Rudia nywila uliyoweka kwenye hatua ilyopita halafu bonyeza OK kwa mara nyingine tena na hapo utakuwa umeiwekea ulinzi nyaraka husika kwa kutumia nywila.
Kama unatumia Ms. Word 2007 kwenye kompyuta basi hatua za kufuata ni kwenda kwenye File > Prepare > Protect Document > Encrypt with Password. Maelezo yanayofuata baada ya hapo yanafanana na hayo niliyoyaeleza awali.
ANGALIZO! Kila kitu kina faida na hasasra zake sasa unaweza ukafurahi kuwa umeweza kuweka nenosiri kwenye nyaraka lakini kumbuka UKISAHAU NYWILA haitawezekana tena wewe kuweza kuiona bila ya kuifungua kwa aina hiyo ya ulinzi.
Chanzo: Microsoft
One Comment
Comments are closed.