Unapobadili kifaa chako ni muhimu kuhamisha taarifa zako kutoka kifaa cha zamani kwenda kifaa kipya, hasa kwa WhatsApp wengi mnaweza kujiuliza namna ya kuhamisha WhatsApp chats kutoka Google Drive kwenda iPhone.
Google Drive ni sehemu ambayo mawasiliano yetu ya WhatsApp (chats) kwa watumiaji wa simu za Android hutunzwa (backups), pia ni ngumu sana kupakua (download) hayo mawasiliano kwa njia ya kawaida, ila ni rahisi sana kufuta haya mawasiliano (delete) au kuzuia yasitunzwe (disable backup) ila siyo kupakua (download chats).
Kwa bahati mbaya ni kwamba hakuna njia ya moja kwa moja ya kuhamisha Whatsapp chats kutoka Android kwenda iPhone mpaka upakue(download) program nyingine kama iCareFone Transfer(iCareFone for WhatsApp Transfer) kwa sababu WhatsApp haitoi huduma ya kuhamisha mawasiliano yaliyotunzwa (chats history) kutoka Android kwenda iPhone.
Unaposakinisha (Install) WhatsApp kwenye iPhone yako kuna namna moja tu ya kurudisha mawasiliano nayo ni kutumia iCloud Je, kama ulikuwa unatumia Android hapo awali itakuwaje?
Namna ya kuhamisha WhatsApp chats kwa kutuma iCareFone Transfer(iCareFone for WhatsApp Transfer)
- Pakua (download) na kisha sakinisha (install) iCareFone Transfer(iCareFone for WhatsApp Transfer)
- Fungua iCareFone Transfer(iCareFone for WhatsApp Transfer) kisha chagua “WhatsApp” kwenye ukurasa wa nyumbani (Home screen) kisha bofya “Backup” iliyopo upande wa chini kushoto kwenye ukurasa wako, baada ya hapo bofya “Download WhatsApp backup from Google Drive to the computer”.
- Ili kuendelea itakulazimu kuingia kwenye akaunti yako ya Google Drive kwa kuweka nywila (password).
- Chagua WhatsApp backup ili kupakua WhatsApp kutoka akaunti yako ya Google Drive.
- Baada ya kupakua (download) chats, programu hiyo itakulazimu kuruhusu akaunti yako ya WhatsApp kwenye simu ya awali.
- Baada ya hapo utaona taarifa zako za WhatsApp (WhatsApp chats), unachagua kuhamisha kwenda simu yako mpya ya iPhone yenye iOS (restore to iOS device).
- Baada ya hapo utakuwa umekamilisha zoezi la kuhamisha WhatsApp chats kutoka simu ya Android yenye Google Drive kwenda simu ya iPhone.
No Comment! Be the first one.