Kama ni mtumiaji wa kompyuta/Computer utakuwa umekutana na maneno kama HDD (Hard Disk Drive) au SSD (Solid State Drive), Hizi ni teknolojia zinazotumika katika kuhifadhi taarifa (Storage) kwenye kompyuta. SSD (Solid State Drive) ni teknolojia ya kisasa zaidi inayotumika kwenye kompyuta za kisasa, na HDD (Hard Disk Drive) ni teknolojia iliyokuwepo kwa mda mrefu.
Kompyuta inayotumia SDD (Solid State Drive) ina kasi kubwa katika kuchakata taarifa tofauti na kompyuta yenye HDD (Hard Disk Drive), pia kompyuta yenye SSD (Solid State Drive) huuzwa ghali kuliko kompyuta yenye HDD (Hard disk Drive).
Unaweza kutumia kompyuta yako kwa mda mrefu na usijue aina ya uhifadhio (storage) iliyopo kwenye kompyuta husika kama ni SSD au HDD.
Baada ya kuyaona hayo sasa utawezaje kujua kama kompyuta yako inatuma SSD au HDD.
kwenye kompyuta yako bonyeza ” Window button +s ” au Bonyeza search bar kwenye taskbar kama inavyoonekana hapa chini.
Ukiwa kwenye sehemu ya kuandika, Andika neno “defrag” kisha chagua “Defragment & Optimize Drives”
Baada ya hapo utaona orodha ya vihifadhio (Drives) zikiwa zimeonyesha kama ni SSD (Solid State Drive) au kama ni HDD (Hard Disk Drive).
Hii ni njia nzuri na nyepesi ya kujua kama kompyuta yako inatumia SSD au HDD, ni muhimu kuelewa kompyuta yako inatumia vifaa vya namna gani, au hata kabla ya kununua ni vizuri kujua baadhi ya vitu kwenye kompyuta hasa hasa huu upande wa teknolojia ya kuhifadhi taarifa.
No Comment! Be the first one.