Unaweza ukamtumia mtu picha na ukashangaa anajua sehemu ulipo, ni kitu ambacho wengi wanashindwa kujua inatokeaje.
Njia mojawapo ya kujua sehemu/location ya mtu pasipo kumuuliza moja kwa moja alipo ni kumwambia atume picha ya kitu chochote alipo,unaweza kumwambia mtu nataka ninunue saa kama yako piga picha nione saa yako.
Unapokua unapiga picha, kinachokua kinahifadhiwa sio sura ya mtu au kitu peke yake ,vitu vingi hua vinahifadhiwa moja wapo ya kitu kinachohifadhiwa ni sehemu/location ya ilipopigwa hiyo picha na hizi taarifa kitaalamu zinaitwa EXIF data ambazo zinajumuisha muda na tarehe, aina ya kifaa kilichotumika kupiga hio picha kama ni simu au kama ni camera DSLR, shutter speed pamoja na white balance na vingine vingi tu ambavyo huwa vinahifadhiwa kwenye picha husika.
Mtu anatakiwa atume picha kwa njia zifuatazo ili uweze kuona sehemu/location yake alipo.
- Atume kama file kupitia WhatsApp
- Atume picha kupitia email
- Atume kwa AirDrop
- Atume kwa Bluetooth
Unaweza ukamwambia atume kama document kwenye WhatsApp ili isipoteze ubora/quality
Kwa watumiaji wa Android
Bonyeza vi doti vitatu kulia juu > bofya details > hapo utaona sehemu/location ya alipopigia hiyo picha.
Kwa watumiaji wa iPhone au vifaa vya Apple
Ukifungua picha bofya kwenye alama ya info, ni herufi i iko kwenye duara kama picha inavyojieleza hapo chini utaweza kujua sehemu/location alipo mpaka aina ya kifaa kilichotumika kuchukua hio picha.
No Comment! Be the first one.