Unaweza ukatumiwa ujumbe kwa njia ya WhatsApp lakini huo ujumbe ukawa umefutwa kabla ya kuusoma, hii inaleta maswali mengi ambayo wengi tunakuwa na shauku ya kujua ulikuwa ni ujumbe wenye maana gani na hasa ikitokea aliyekutumia ujumbe asikwambie alitumia ujumbe wenye maana gani.
Hili andiko ni kwa watumiaji wa simu zenye programu endeshi ya Android (smartphones with Android OS), kuna namna kuu mbili za kufanya ili uweze kuona jumbe/messages zilizofutwa pasipo kuzisoma kupitia WhatsApp.
- Fungua sehemu ya mipangilio (Settings) kwenye WhatsApp.
- Nenda kwenye sehemu ya notifications
- Bofya kwenye sehemu ya advanced settings
- Angalia na ubofye sehemu ya notifications history
- Hapo ruhusu/washa “turn it on
Hapo utapata notifications zote, utakuwa unaziona hapo hata zile messages ambazo mtu hufuta kabla ya wewe kuziona.
Kama njia ya kwanza haijafanya kazi basi itabidi utumie Programu/Apps ambazo zitakusaidia kurahisisha hili zoezi. Programu/Apps kama WAMR, WhatsTool amabzo inabidi uzipakue/download.
Picha hizi ni Program/App ya WhatsTool, inakupasa ukishaipakua na kuiweka kwenye simu (Install) utakubali (Allow) ili iweze kufanya kazi vizuri kwenye simu husika, baada ya kukubali nenda kwenye sehemu ya “recover deleted messages” Fuatisha melekezo kama picha zinavyoonesha.
Ukiruhusu itafungua sehemu ya “Start recovering Message” na utaruhusu kisha App itaanza kutafuta na kurudisha/recover jumbe za ambazo zilifutwa pasipo kuzisoma.
Watu wengi huachwa na maswali mengi pindi wanapokuta ujumbe umefutwa kwenye WhatsApp kabla hawajausoma, lakini pia kuna njia rahisi za kuweza kusoma hizo jumbe ili kuridhika au kujua ni kitu gani kilitumwa, hii njia ni kwa watumiaji wa simu zenye programu endeshi ya Android (Smartphone with Android OS).
No Comment! Be the first one.