
Watumiaji wengi wa simujanja/smartphones zenye programu endeshi ya Android (Android smartphones) wamekutana na tatizo la simu zao kusumbua au kutokubali kuunganishwa na kompyuta kwa kutumia waya (USB cable) ili waweze kuhamisha faili baina ya simu na kompyuta.
Hili ni tatizo linaloleta kero na adha kubwa kwa watumiaji na mara nyingi wamejikuta kukerwa na aina ya simu wanazotumia, kuna njia nyingi za kutatua hili tatizo.
1. Angalia Mipangilio/settings za USB (Check USB computer connection settings).

Kuweza kusafirisha taarifa kati ya simu na computer kupitia USB unatakiwa kuweka simu kwenye MTP mode (Media Transfer Protocol)
Fungua simu yako nenda kwenye mipangilio/settings > bofya storage > bofya kwenye alama ya “more” (juu upande wa kulia) > Chagua USB computer connection > kwenye orodha chagua Media device (MTP)
2. Ruhusu USB Debugging (Enable USB debugging)

Hii njia inasaidia kwa kiasi kikubwa tatizo la simujanja kushindwa kusoma kwenye kompyuta
> Nenda kwenye Mipangilio/settings ya simu yako > bofya kwenye “developer options” > weka developer options ON na ubofye OK( switch on and click OK) > angalia USB connection na uiruhusu (check USB debugging and enable it)
Namna ya kupata Developer options kama haipo kwenye simu yako.
Nenda kwenye settings ya simu > angalia na ufungue about phone > bofya kwenye build number na ubonyeze mara 7 utakuwa umepata developer options kisha enable USB debugging.
3. Weka MTP drivers kwenye kompyuta yako (Install MTP USB device drivers )

Wakati mwingine tunahitaji kufanya masasisho (updates) ya drivers kwenye kompyuta zetu.
Right click “This PC” > bofya “Manage” > nenda kwenye “Device Manager” > Hapo utaona orodha ya drivers nyingi > Nenda kwenye portable (MTP) device driver > right click kisha chagua “update driver software”
- Chagua “browse my computer for driver software”
- kutoka kwenye orodha chagua “MTP USB device” > bofya next > sakinisha/install driver na kifaa chako kitasoma kwenye kompyuta.
4. Weka simu kwenye airplane mode.
Hii pia inasaidia, unaweza kuweka simu kwenye airplane mode ukabadilisha faili kati ya simu na kompyuta na ukimaliza unatoa airplane mode.
5. Futa vitu vya akiba na uianzishe upya simu (Clear cache and restart your android phone)

Nenda kwenye mipangilio wa simu yako (phone settings) > Nenda kwenye aplikesheni/apps > bofya vidoti kwenye kona kulia kisha chagua “show system apps”
- Chagua “external storage and media storage apps” kisha futa/clear cache pamoja na data
- Ukimaliza hapo anzisha upya simujanja yako (restart your smartphone)
No Comment! Be the first one.