Facebook huingiza kipato kutokana na matangazo, lakini matangazo hayo yanapoendelea kuwa mengi na kuonekana kwenye ukurasa wako huwa yanakera. Ni kweli Facebook haitaki matangazo hayo yaondolewe na hakuna mwongozo rasmi au program ya kuyaondoa.
Ili kuodoa hayo matangazo unahitaji kupakua (download) program ya kuondoa matangazo (ad-blocking) au unahitaji kuboresha mipangilio (update settings) kwenye ukurasa wako.
Unapobofya “like” kwenye bidhaa au tangazo au ukurasa flani, Facebook hutumia taarifa zako kama Jina, sehemu ulipo kuonyesha tangazo/matangazo hayo kwenye kurasa za marafiki zako, hii pia inakuwa haiko vizuri hasa kwenye usiri wa taarifa binafsi ( Information privacy). Wafanyabiashara na watu binafsi hutumia Facebook kutangaza bidhaa au huduma zao na unaweza kuwa umeshuhudia pindi unapotafuta bidhaa flani kwenye kivinjari cha Google (Google search) na ukakuta tangazo la bidhaa hiyo limeweka limewekwa kwenye ukurasa wako wa Facebook.
Huwezi kuchagua kutoona matangazo ya Facebook kabisa, lakini unaweza kuchagua kutopokea matangazo
kulingana na tabia zako au vitu unavyopenda kuvitembelea mara kwa mara mtandaoni.
Ili uweze kupunguza au kuzuia matangazo, fanya yafuatayo.
1. Ingia kwenye ukurasa wako wa Facebook, kisha bofya “Settings” kwa sasa unaweza kuipata kwa kubofya
kwenye vidoti vitatu chini ya picha yako ya jarada (Cover photo) kisha nenda kwenye “Profile and Tagging Settings”
kutokea hapo utaona Settings.
2. Ukiwa sehemu ya Settings, shuka chini utaona sehemu ya Matangazo (“Ads”) ukibofya hapo utaona
maelekezo mbalimbali ya matangazo (ad preferences).
3. Ukiwa kwenye sehemu ya “ad preferences” utaona machaguo matatu ya matangazo (three options)
ambayo ni “Advertisers,” “Ad Topics” na “Ad Settings. Kwenye upande wa Advertisers utaona makampuni
ambayo huweka au kuonyesha matangazo kwenye ukurasa wako, hapa kuna sehemu ya kuficha haya
matangazo kwa kubofya “Hide Ads.”
4. Kwenye upande wa “Ad Topics” inkuwezesha kuona matangazo machache kulingana na vitu au
mada unazozipenda, mfano mada za wanyama, michezo n.k. Bofya kwenye “Show Fewer” kwenye kila
mada/topic husika.
5. Kwenye upande wa “Ad Settings” hii inakupa matangazo kulingana na taarifa zako binafsi
(personal information) mfano taarifa zako za elimu, mahusiano yako n.k. Mipangilio hii (settings)
inaweza kurekebishwa ili kupunguza idadi ya matangazo yanayokufaa kuyaona, lakini siyo idadi ya
matangazo yatakayooneshwa kwenye ukurasa wako. hapo unaweza kuzima (off) kwa kila mipangilio
(settings), ukizima unaondoa kile kitufe cha blue kinakuwa cha kijivu.
Matangazo yakiwa mengi kwenye ukurasa wako wa Facebook huwa yanakera na kuondoa hamu ya kutumia huo mtandao, hizo hapo juu ni baadhi ya njia za kupunguza matangazo ili uweze kutumia Facebook vizuri bila kero yoyote.
Unaweza pia kusoma makala zetu zingine hapa.
No Comment! Be the first one.