Teknolojia nyingi mpya zinazogundulika kwa sasa za kuboresha uwezo wa mabetri ya simu n.k zimekuwa ni teknolojia zinazoonesha kuwa ni ghali na zitachukua muda kuleta bidhaa sokoni ila hii iliyogundulika sasa ni bora zaidi kwani inaboresha teknolojia inayotumika tayari kwa mabetri ya Lithium-ion.
Kila ugunduzi mpya ukifanyaika katika eneo la teknolojia ya mabetri huwa ni habari inayopokelewa kwa furaha sana na sasa wanasayansi nchini Marekani wamegundua njia ya kuboresha teknolojia ya mabetri yanayotumika sana kwa sasa – ya lithium-ion.
Muda mwingine kuchezea chezea vitu ovyo kunaweza kuwa na manufaa!
Ugunduzi huu ambao inasemekana ulifanyika bila ata kupangiliwa (watafiti wanasema waligundua jambo hili wakati wakiwa wanajaribu jaribu tuu kucheza na teknolojia ya ‘nanowires’). Watafiti hao ni wa Chuo kikuu cha Calfornia tawi la Irvine huko nchini Marekani.
Kupitia utumiaji wa waya spesheli za ‘nanowires’ ndani ya mabetri wamegundua betri litaweza kuduma kuchajiwa mara nyingi sana bila kuathiri uwezo wake wa kuhifadhi chaji.
Nyaya za nanowires zilishafikiliwa hata miaka ya nyuma ila wengi walishaone haitawezekana kutumika kutokana na mapungufu kadhaa ambayo Bwana My Le Thai ameweza kuyatatua kwa kufunika nyaya hizi na ngozi ya madini ya dhahabu na kisha kufunika na ‘manganese dioxide’ na kisha ndani ya betri kuwa na mafuta spesheli ya athiri ya gel. Kwa hatua hizi betri linaweza dumu miaka mingi sana ukilinganisha na mabetri ya sasa.
Wanamaanisha nini hasa?
- Kwa kawaida kwa sasa betri zinazotumika ata kwenye simu na vifaa vingine vya elektroniki ni za teknolojia ya lithium-ion.
- Betri hizi zinaweza himili kuchajiwa mara elfu 5, nyingine elfu 6 na kiwango cha juu kabisa kikiwa 7,000. Baada ya hapo betri litakuwa tayari lipo chini ya kiwango katika suala la utunzaji chaji, na dalili moja wapo ni kuanza kuvimba.
- Kupitia teknolojia spesheli waliyoigundua ya kutengeneza betri hizo ambapo nanowires (ambazo ndio vitunza chaji) zinazungukwa na gel spesheli…betri litakuwa na uwezo wa kuhimili hadi kuchajiwa zaidi ya mara 100,000 kabla ya kuanza kupoteza ovyo chaji yake.
Kwa sasa kuboresha teknolojia ya betri ni jambo linalopewa kipaumbele sana kwani wakati vifaa kama vile simu, tableti na vingine vikizidi kupata uwezo mkubwa katika utendaji kazi lakini bado suala la betri zake kuwahi kuisha chaji na kuharibika limekuwa ni changamoto kubwa.
Soma makala zetu zingine zinazohusu teknolojia za betri -> Teknokona/Betri
Chanzo: ComputerWorld
One Comment
Comments are closed.