Kutokana na ukuaji wa teknolojia NASA imekuwa sehemu ya kutafuta ubunifu mpya ambao hautumi nguvu kazi nyingi bali teknolojia na kuleta matokeo chanya.
Dunia ina majanga mbalimbali ya asili ambayo yanafanya watu kuweza kufikiria ili kupata njia sahihi ya kukabiliana nayo na hata kuwa na uwezo wa kupunguza madhara kabla ya jambo lenyewe kutokea. NASA ipo mbioni kutengeneza ndege ambazo haziendeshwi na rubani (drones) ambazo zitakuwa na uwezo wa kutambua uwezekano wa kutokea volcano mahali husika.
Katika kulifanikisha hilo NASA inashirikiana na kiwanda cha kutengeneza ndege hizo kilichopo Colorado-Marekani ambapo watatenegeneza mfumo wa kutumika kwenye ndege zisizokuwa na rubani kuweza kupata taarifa za kitaalamu kuhusu uwezekano wa kutokea volcano mahali husika.
Hii sio mara ya kwanza kwa NASA kufanya kitu kama hiki
Mwaka 2013, NASA kwa mara ya kwanza ilitengeneza ndege za mtindo huo ambazo zilitumika kusaidia kukabiliana na volcano ya Turrialba huko Costa Rica. NASA pia imekuwa kwenye ubia wa muda mrefu na Black Wing Technologies ambayo inajihusisha na utengenezaji wa mifumo ya kutumika kwenye ndege zisizokuwa na rubani zenye kuhimili maeneo ambayo ni magumu kufikika kutokana na sababu mbalimbali.
HAta hivyo, ndege hizo hazitakuwa na uwezo wa kujua uwezekano wa kutokea maafa yanayoanzia chini ya maji kama yale yaliyotokea Hunga-Tonga lakini kazi ambayo zitasaidia wanasayansi kutoa taarifa mapema kabla ya kutokea volcano.
Vyanzo: 9to5Google na mitandao mbalimbali
One Comment