NASA ni shirika la utawala wa Anga ambalo linahusika na maswala yote yanayohusiana na anga huko nchini marekani. Shirika hili ni moja kati ya mashirika makubwa kabisa na yenye heshima sana duniani.
Habari hii imetolea na NASA wenyewe hapo ijumaa na wamesema huduma hii ya ku’stream itaanza kupatikana mwaka huu na itakua inakwenda kwa jina la NASA Plus.
Huduma hii inaanzishwa na shirika mahususi kabisa katika kuhakikisha kuwa inarusha mambo kadha wa kadha ikiwemo safari zake za anga na vipindi tofauti tofauti ambavyo vinahusiana na mambo hayo.
Hawakuishia hapo tuu pia kumbuka wana maktaba (kumbukumbu) nyingi ambazo watakua wanazirudha kupitia katika huduma hiyo mpya ya ku’stream.
Kingine ni kwamba kutakua na maudhui mapya amabayo yatakua yanazalishwa kwa ajili ya watazamaji kwa wakati huo licha ya kwamba kutakua na maudhaui mahususi kutoka NASA (NASA Original).
Huduma za ku’stream kwa sasa ziko nyingi sana na kwa makampuni mengi hii ni njia nzuri ya kupata hela maana mara nyingi huduma hizi huwa zinakua ni za kulipia.
Mpaka sasa inajulikana kwamba NASA Plus itakua ikipatikana bure kabisa na itakua pia ikipatikana katika huduma za Apple TV, Fire TV and Roku bila kusahau app yake ya Android na iOS.
Baadhi ya vipindi (mfululizo wa vipindi) ndani ya NASA Plus itakua ni NASA Talks, Space Out, The Color of Space, NASA Kids, NASA Explorers, WEBB Space Telescope, First Light, NASA En Español, Lucy, Mars Is Hard, NASA Explorers: Osiris Rex and Artemis I: Path to the Pad n.k
NASA Plus itakua ni bure kabisa kama nilivyosema na itakua ni huduma ambayo haina matangazo –hii ni kwa mujibu wa NASA wenyewe.
NASA pia wameweka wazi malengo yake yajayo ambayo yanahusisha kuweka sasisho (update) katika App yake na tovuti (website) yake.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unahisi huduma hii kutoka NASA itpata watazamaji wengi kama huduma zingine? Na je watakuja kutoza watu au kuweka matangazo?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.