Kampuni ya Netflix sio ngeni katika ulimwengu wa magemu maana mpaka sasa kwa kupitia App yake ya Android na iOS huduma za magemu zinapatikana humo.
Mpaka sasa Netflix ina magumu ya kutosha na hili linawafanya waingie katika soko hili wakiwa kifua mbele. Kama unakumbuka tulishawahi kuandika kuhusiana na Netflix kuinunua kampuni ya kutengeneza magemu >>HAPA<<
Ni wazi kwamba kampuni mpaka sasa inataka kwenda mbali zaidi na huduma yake ya magemu kwa maana kwamba hawataki kubakia katika simu tuu (Android na iOS).
Netflix inakuja na magemu haya katika mfumo wa ku’stream na zitakuja katika vifaa kama vile TV na hata kompyuta
Kwa kupitia huduma hii ya ku’stream watu watakua na uwezo mkubwa wa kucheza magemu hayo kupitia kifaa chochote kwa wakati wowote na kuendelea kufurahia magemu hayo.
Kizuri hapa ni kwamba utakua na uwezo wa kucheza magemu haya katika vifaa vingi zaidi licha ya kuwa na uwezo wa kucheza kupitia simu yenyewe pekee.
Kitu cha kuzingatia hapa wakati ukiwa unacheza magemu haya kupitia TV au kompyuta ni kwamba ni lazima uhakikishe una kifurushi cha intaneti cha kutosha – pengine inawezekana ikawa inakula zaidi kuliko kutazama vipindi vya Tv/Filamu.
Kizuri ni kwamba kutakua hakuna gharama ya ziada kwa maana ya kwamba utatumia kifurushi hicho hicho bila kuongezeka gharama katika kuhakikisha unatumia huduma hii.
Huduma hizi zitaanza kupatikana kote kwa watumiaji wa Smart TV na katika mtandao
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.