Moja kati ya mtoaji mkubwa wa huduma ya ku’stream, Netflix imekuja na kipengele kingine kwa ajili ya watoto na hiki kimeanza kupatikana kwa watumiaji wa Android tuu.
Netflix sio mara ya kwanza kufanya maboresho katika huduma yake, ni mara kwa mara huwa wanakuja na vipengele vipya au kufanya maboresho katika vile ambavyo vipo ili tuu kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata kile kilicho bora.
Kipengele hiki ni mahususi kabisa kwa maudhui ya watoto, hii inakua ni tofauti kabisa na maeneo mengine ambayo huwa yanakua na maudhui ya aina nyingi mfano ya kikubwa.
Ili kufurahia kipengele hiki watoto, wazazi au hata walezi itawabidi waingine katika akaunti ya motto ndani ya mtandao wa Netflix ili kufurahia maudhui ya humo.
Kwa haraka haraka ni kwamba eneo hilo –Kids Mystery Box—litakua na kazi ya kutoa pendeko la maudhui kadhaa kwa ajili ya kangaliwa na watoto.
Mara kwa mara mitandao ambayo ina maudhui ya aina mbali mbali imekua ikifanya juu chini katika kuhakikisha kuwa inatenga maudhui hayo kulingana na umri wa wateja wao.
Hii ni moja wapo ya njia za kampuni ya Netflix katika kuhakikisha kuwa wanafanya juu chini katika kuhakikisha kila mtu anapata maudhui stahiki.
Mwaka 2021 kampuni iliandaa kipengele cha ‘Kids Top 10 Row’ ambacho kilikua ni mahususi kwa ajili ya kuonyesha maudhui kumi ya watoto.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani kipengele hiki ni kizuri sana kwa watoto na kuna udhibiti wa hali ya juu kwa wao kutokwenda katika maudhui mengine.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.