Ushawahi kufikiria uwezekano wa uwepo wa nguo zinazojisafisha zenyewe? Yaani suala la kufua linakuwa historia..wanasayansi wamefanikiwa kutengeneza marighafi ya nguo yenye uwezo wa kujisafisha yenyewe na kujitoa uchafu pale inapopata mwanga.
Marighafi (textile) hiyo ya nguo imechanganywa na vidude vidogo (nanostructures) vyenye uwezo wa kuvunja vunja kitu chochote kilicho ‘organic’ (yaani kikaboni/kilichotoka kwenye kitu kilichokuwa hai).
Uvunjaji huo unaotokea pale marighafi hiyo inapokutana na mwanga ndicho kinacholeta usafi kutokea, kwani uchafu uliokuwa umekaa kwenye nguo usika utakuwa umevunjwa vunjwa na hivyo kupotea – kupitia kuanguka – kupeperuka n.k.
Huu ni utumiaji wa teknolojia ya Nano (Nanotechnology), ambayo kwa kutengeneza vitu viduchu vinavyoweza changanywa na ‘material’ ya nguo. Mwanga wa taa au jua utasababisha nguo ianze kuuharibu uchafu wowote ulio juu yake.
Wanategemea kutengeneza vitambaa kwa ajili ya kushonea nguo vya pamba vitakavyokuwa vimechanganywa vizuri na mjumuiko wa ‘nanostructures’ zenye uwezo wa kujisafisha pale zinapopata mwanga.
Wanasema ni mapema mno kuona nguo za namna hizo zikipatikana madukani ila ni teknolojia wanayoifanyia kazi na tayari ni jambo linalohusu maboresho zaidi. Hasa hasa kuzidi kuhakikisha pia gharama za teknolojia hiyo zinakuwa ni za chini tuu.
Teknolojia hii inatengenezwa na timu ya wanasayansi wa chuo cha nchini Australia – RMIT University.
Je unamaoni gani juu ya teknolojia hii ya nguo zinazojisafisha zenyewe?
Soma pia – LAUNDROID: Panasonic Waja na Roboti kwa Ajili ya Kufua, Kukunja na Kupanga Nguo
Chanzo: IBTimes UK na vyanzo vingine mbalimbali