Mtandao wa kijamii wa Twitter kama ilivyo mingine mtu anaweza akatumia kupitia kivinjari kwa kutembela tovuti au kifaa chake cha kiganjani ambacho kinaweza kutoka kwenye programu endeshi mbili maarufu.
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamegawanyika kutokana na kuwepo mitandao lukuki ya kijamii na hivyo kumpa mtumiaji uwanja mpana wa kuchagua wapi aende afungue akaunti ili awezw kuperuzi halikadhalika kuwailiana na marafiki atakaowapata/wakuta huko.
Mtandao wa kijamii wa Twitter tangu kuanzishwa kwake haujawahi kuwa na watumiaji wengi kuzidi Facebook au hata hiyo mingine ambayo ina watu lukuki na hata kuwafanya watu kuwa na uraibu wa kushindwa kupitisha muda fulani/siku bila ya kuperuzi huko. Je, wewe mtumiaji wa Twitter kwenye Android ulishwahi kutaka kunakili sehemu fulani ya chapisho la mtu na ikashindikana? Najua jibu ni ndio tuu.
Kwa wanaotumia Twitter kwenye Android kipengele kipya kinafanyiwa kazi ambacho kitamuwezesha mtumiaji kuweza kuchukua sehemu fulani ya maandishi kwenye chapisho la mtu na kuweza kulinakili, kusambaza, n.k kama ambavyo imekuwa ikiwezekana kwenye iOS kwa muda mrefu tuu.
Habati hii ni ya kufurahisha hasa ukizingita kitu hicho kimekosekana kwenye mtandao huo wa kijamii kwa upande wa Android kwa muda mrefu tuu lakini wakati wao sahihi unawadia. Waswahili husema “Lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja”.
Vyanzo: Pro Pakistan, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.