Dola bilioni 62.3 ni nyingi sana kwa dunia ya sasa kwa kitu chochote, Nintendo kupitia Nintendo switch wameweza kuingia kiasi hicho cha pesa kama sehemu ya mapato.
Mapato hayo yamewekwa wazi kuwa yamepatikana katika Nintendo Switch tuu kwa vifaa vyake vya softaware, hardware na mambo mengine kama vile huduma zake za kulipia hii inaweza ikawa ni kwa baadhi ya magemu yake n.k.

Mapato haya yameanza kuhesabiwa kuanzia mwaka 2017 na kwa switch peke yake maana ukiangalia kampuni ya Nintendo ina mambo mengi sana ambayo yanawaingizia pesa.
Kuna ripoti ambayo imetolewa na mtandao wa Nintendo ambao umeweka wazi taarifa zote hizo za mapato umeonyesha ni jinsi gani kampuni imeweza kujipatia mapato kupitia sehemu moja tuu.

Nintendo Switch zipo za aina nyingi na zote zilifanya vizuri katika soko, sababu kubwa ikiwa ni zilikuja kwa utofauti na soko lilivyokua likitegemea.
Kwa sasa katika nyanya ya magemu hata katika vifaa vya magemu imeonekana dhahiri kwamba makampuni haya huwa yanaingiza pesa nyingi sana ukilinganisha na mengine.
Kingine cha kushangaza ni kwamba magemu katika simu ndio yanaongoza kukusanya mapato mengi ukilinganisha na magemu katika maeneo mengine.

Ripoti hii ni ya tokea mwaka 2017 ambapo kila robo mwaka kampuni ya Nintendo ilikua inaweka wazi mauzo yake ya miezi mitatu mitatu kwa mwaka nzima, jumla yake ndio kinakuja kiasi hicho cha hela
Ningepesa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika sehemu ya maoni, je unahisi kwa kupitia Nintendo nzima unadhani kampuni itakua imetengeza bei gani?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.