Nintendo ina sifa kubwa sana kwa upande wake wa teknolojia ya magemu na teknolojia zingine.
Gemu ambalo ni maarufu sana ambalo linamilikiwa na kampuni ya Nintendo ni Super Mario.
Chapa ya Super Mario imeleta faida kubwa sana katika kampuni hali ambayo inalifanya kampuni kuwa kifua mbele katika tasnia ya magemu.
Licha ya kuwa na umiliki wa magemu mengi kwa sasa kampuni imeamua kuachia gemu ya bure katika mtandao.
Gemu linajulikana kama Pikmin Finder na ili kulicheza inabidi utumia kivinjari cha simu na kuingia >>HAPA<<
Au unaweza kuingia moja kwa moja kwa kuandika pikmin-finder.nintendo.net katika kivinjari chako cha simu.
Cha kufurahisha ni kwamba gemu hili ni ushirika wa makampuni mawili ikiwemo Niantic na Nintendo.
Gemu hili linaongozwa na Teknolojia ya AR, na litachezwa kwa vifaa vya mkononi tuu kama vile simu janja na tabiti huku likitumia vivinjari vya vifaa hivyo.
Kwa haraka haraka ni kwamba teknolojia iliyotumika katika Pokemon Go ndio imetumika katika uandaaji wa gemu hili.
Ni wazi kwamba kwa sasa masoko ma magemu yanafanya vizuri sana kwa kawaida magemu huwa yaningiza mapato makubwa sana ukilingnaisha na masoko mengine ya burudani.
Nintendo mara kwa mara imekua ikishirikiana na makampuni mengine kadha wa kadha katika kuhakikisha kuwa wanakuja na magemu pendwa kwa wateja na watumiaji wake
Ningependa kusikia kutoka kwako, gemu hii ni ya bure kabisa je uko tayari kuanza kuicheza? Niandikie hapo chini katika sanduku la maoni
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.