Bodi ya kuratibu vyakula na madawa (Food and Drugs Administration) ya nchini Marekani imepitisha matumizi(ya kiraia) ya bomba sindano (lenye vi-sponge) kwaajiri kuzuia kuvuja damu katika majeraha ya risasi , njia hii ambayo ni teknolojia mpya kabisa katika sekta ya afya na tiba ilitengenezwa kwaajiri ya kutumika jeshini.
Teknolojia hii mpya inatumia sponge ndogo ndogo ambazo zinawekwa ndani ya kitu kama bomba la sindano, vi-sponge hivyo humwagwa katika jeraha la risasi kwa namna ile ile ambayo dawa hutolewa kutoka katika bomba la sindano.
Vi-sponge hivyo vimetengenezwa kwa kutumia cellulose vinauwezo wa kutanuka muda mfupi baada ya kugusa damu ama kimiminika, kutanuka kwake huvifanya viweze kujaza eneo lile la kidonda vilipomwagiwa na kusaidia kuzuia damu kuendelea kutoka.
Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi watu wengi wanaokufa kwa majeraha ya risasi hufa kwasababu wanapoteza kiwango kikubwa cha damu kabla ya kufikishwa hospitali ambako wangepatiwa huduma ya kuzuia damu kuvuja.
Bomba moja la sindano linaweza kunyonya kiasi cha karibu nusu lita cha damu, na mtu mmoja anaweza kutumia mabomba matano ya vi-sponge hivyo. Kila ki-sponge kinakuwa na tag maalumu inayotumika kuhakikisha kwamba kila ki-sponge kimetolewa mwilini.
Huduma hii ambayo imepewa jina la Xstat Rapid Hemostasis System ni habari nzuri kwa nchi nyingi ambazo zina matukio mengi ya vurugu za bunduki kama Marekani, hii ni hatua moja mbele kwa teknolojia kubadilisha maisha yetu ya kila siku.
Endelea kutufuata katika mitandao ya kijamii Twitter Facebook na Instagram ili ujipatie habari za teknolojia kwa lugha ya kiswahili pindi tu zinapotokea.
No Comment! Be the first one.