Huduma ya kuweka namna za siri kwenye kadi zetu za simu limekuwepo kwa miongo mingi tuu halikadhalika wengi tuu waliachana na matumizi kadi fulani ya simu kutokana na kupoteza namba za PUK!
Mimi ni mmojawapo wa watu ambao nilikuwa napata changamoto sana tuu hasa pale ambapo nilikuwa nasahau namba za PUK ama kwa namna moja au nyingine nimepoteza ile kadi ya simu ambayo inakuwa na namba za siri (PIN), namba za kuweza kufungua kadi ya simu mara mtu anapokosea namba ya siri.
Miaka mingi baadae mambo yamebadilika, teknolojia imekuwa kiasi kwamba mtu anaweza kupata namba za PUK kwa kuwasiliana na huduma kwa wateja kisha kufuata maelekezo husika kuweza kuanza hatua ya kufungua kadi yake ya simu. Hicho ni kitu kizuri lakini kilichonivutia zaidi ni njia rahisi ya kupata namba za PUK bila kupiga namba ya huduma kwa wateja.
Tigo Tanzania wameongeza kipengele kipya kwenye menyu ya *147*00# kisha kuchagua “Language/Huduma kwa wateja”>>Pata PUK>>Utaweka tarakimu kumi za namba yako ya simu>>Kuweka namba zako za NIDA baada ya hapo utapokea ujumbe mfupi wa maandishi ukiwa namba za PUK (Personal Unblocking Key) zinazohusu namba ya simu husika.
Urahisi wa kupata namba za kufungua laini kwenye simu ya kiganjani.
Si Tigo Tanzania pekee ndio wana huduma hii bali hata mitandao mingine ya simu lakini msingi wa huduma ni mhusika kuwa na NAMBA YA NIDA. Sasa hofu isiwepo tena mara unapokosea namba ya siri ya kwenye kadi ya simu.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
Nafikri Voda wana huduma ya mteja kujihudumia mwenyewe kuhusu namna ya kupata PUK lakini ambacho nina uhakika nacho ni lazima utaombwa namba za NIDA ulizotumia kusajili laini husika. Hivyo, tafuta mtu mwingine mwenye laini ya Voda akusaidie kufanikisha huo mchakato.
0623366266
Laini yangu 0755350649 imejifinga insdai puk nafanyaje?
Nafikri Voda wana huduma ya mteja kujihudumia mwenyewe kuhusu namna ya kupata PUK lakini ambacho nina uhakika nacho ni lazima utaombwa namba za NIDA ulizotumia kusajili laini husika. Hivyo, tafuta mtu mwingine mwenye laini ya Voda akusaidie kufanikisha huo mchakato.