Tumeshaandika kuhusu maboresho ya kiteknolojia katika utengenezaji wa barabara za magari, lakini leo fahamu kuhusu km 5 inayotegemewa kufikia km 100 inayojengwa spesheli kwa ajili ya matumizi ya baiskeli.
Njia hii spesheli kwa ajili ya baiskeli inategemewa kujengwa na kuifikia idadi ya km 100 za urefu na itaunganisha miji 10 iliyo eneo Ruhr nchini Ujerumani. Miji hiyo ni pamoja na Duisburg, Bochum na Hamm, na pia katika sehemu hii ya mwanzo ya mradi huo barabara hiyo itapitia pia vyuo vikuu vinne.
Katika urefu huo wa km 5 takribani km 2 kati ya hizo zimepita maeneo yenye takribani idadi ya watu milioni 2 na wakazi hao wataweza sasa kufika maeneo mbalimbali kwa haraka zaidi kwa kutumia baiskeli zao. Kwa sasa inakadiriwa takribani magari 50,000 yatapungua barabarani kwa siku kutokana na watu kuweza kutumia baiskeli kwenye njia hizo spesheli. Na hii itasaidia kupunguza foleni na uchafuzi wa hali ya hewa unaotokana na utumiaji magari.
Utengenezaji wa barabara hiyo spesheli kwa ujumla wake wa km 100 utagharimu zaidi ya Tsh bilioni 420 (Euro milioni 180).
Upo hapo?
No Comment! Be the first one.