Nokia 7 Plus imekuwa ni simu ambayo inazungumziwa na tovuti mbalimbali na wengi kuamini kuwa ndio simu ambayo inaiweka vyema kwenye ramani ya biashara ya simu janja kwa Nokia ambayo ilikuwa imeyumba kabisa.
Mfululizo wa simu za Nokia umekuwa ni wa kufuatana tangu kampuni hiyo iliponunuliwa na HMD Global mwaka 2017 na tangu hapo wametoa simu janja kadha wa kadha lakini sita kati ya hizo wakilenga soko la India na Uchina.
Nokia 7 Plus imekuwa ikizungumzwa sana kwa sababbu kuu mbili; muonekano wake (rangi+madini yaliyotumika kutengeneza mfuniko wa juu) pamoja na nguvu iliyowekwa kwenye betri.
Nokia 7 Plus ambayo rangi yake ya Nyeusi na Shaba inayoonekana kuifanya simu hiyo ya kuvutia.
Sifa nyinginezo za Nokia 7 Plus.
Prosesa & Programu endeshi. Moja kati ya prosesa za kisasa na zenye nguvu kabisa ndio ipo kwenye Nokia 7 Plus; Snapdragon 660 ikiwa na toleo la Andoud 8.1 (Oreo) upande wa programu endeshaji.
Kioo & Kamera. Hapa tunaongelea kioo chenye ukubwa wa inchi 6 ambacho vitu vinaonekana ang’avu kabisa na ukiwa na uwanja mpana wa kubonyeza vitu bila shida. Kwenye upande wa kamera ile ya mbele ina MP 16 na ya nyuma ina MP 13+LED flash, kazi ambayo imefanya na Zeiss.
RAM & Diski uhifadhi. Nokia 7 Plus imewekwa RAM ambayo kwa uhakika hutaona simu yako ni kero katika ufanyaji wake wa kazi, hapa nazungumzia GB 4 kwenye RAM na GB 64 kwenye memori ya ndani kwenye simu. Vilevile, ina nafasi ya kuweka memori ya ziada ya mpaka GB 256.
Betri & Mengineyo. Betri ya kwenye Nokia 7 inauwezo wa kudumu siku moja na nusu kwa matumizi ya simu pamoja na intaneti lakini kama utatumia kwa matumizi ya kawaida tu basi ina uwezo wa kukaa na chaji mpaka siku mbili. Hivyo, kiujumla ina 3800mAh.
Nokia 7 Plus inatumia kadi mbili za simu, ina teknolojia ya kuchaji simu kwa haraka, Wi-Fi, GPS, Bluetooth, NFC, 3G , 4G LTE, alama ya kidole kwa ajili ya usalama.
Nokia 7 Plus inapatikana kwa rangi 2; Nyeupe na Nyeusi lakini zote zikiwa zimezungukwa na utepe wa madini ya chuma ya rangi ya Shaba.
Wakati Nokia Plus inatoka mapema mwaka 2018 ilitoka kwa pamoja na Nokia 6.1 vilevile Nokia 8 Sirocco lakini Nokia 7 Plus imeonekana kuwavutia watu wengi ikipatikana kwa zaidi ya $460|Tsh. 1,058,000.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
One Comment
Comments are closed.